Simu

Simu Mpya za Google Pixel 2 Zimevuja Kabla ya Kutoka (Bei+ Picha)

Kampuni ya Google ambayo ndio watengenezaji wa simu za Pixel hivi karibuni imepata pigo kwa kuvuja kwa picha za simu za pixel 2 ambazo zinasemekana ndio toleo jipya la mwaka huu 2017.

Picha hizo ambazo zimevuja mtandaoni zinaonyesha matoleo yote mawili ya simu za pixel za mwaka huu 2017, kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.

Simu hiyo itauzwa kwa dollar za marekani $649 hadi $749 sawa na shilingi za Tanzania Tsh 1,454,409.00 hadi Tsh 1,678,509.00.

Ripoti zinaonyesha Pixel 2 itatengenezwa na HTC, wakati LG watatengeneza pixel 2 XL.

Kwa mujibu wa tetesi hizo kwa upande wa simu ya Google Pixel 2 XL simu hii inatarajiwa kuja na kioo cha inch 6 huku ikiwa na ukubwa kuanzia GB64 ikiwa na bei ya $849 na nyingine yenye ukubwa wa GB 128 huku ikiwa na bei ya dollar za marekani $949.

Google inatarajiwa kuzindua simu hizi tarehe 4 Oktoba.

SOMA NA HII:  Listi ya Simu 5 za Halotel zinazouzwa kwa bei nafuu kabisa.
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

Toa Maoni Hapa:

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako