Sambaza:

Tecno R7 na Tecno D7 zote zina skrini ya kugusa yenye inchi 5.5 na zinatumia programu endeshi ya Android 4.2.2 (Jelly Bean), lakini hizo ni sifa tu za kufanana kati ya vifaa hivi viwili. Tecno D7 ni phablet ya kiwango cha kawaida wakati Tecno R7 ni kifaa cha juu kwenye suala la utendaji na ni kifaa chenye nguvu ya prosesa mara 3 zaidi na RAM mara 4 zaidi. Zifuatazo ni tofauti kuu kati ya Tecno R7 na Tecno D7.

 

 

 

 

 

 

 

Uwezo wa simu

Kwa 1.3GHz dual-core Tecno D7 hailingani na processor ya 1.5GHz 6-core ya kwenye Tecno R7. Hivyo, tarajia utendaji mzuri kwenye R7. Mapungufu mengine ya Tecno D7 ni kwamba ina RAM ya 512MB tu, Tecno R7 hata hivyo ina uwezo zaidi ya mara 4 kwa sababu ina 2GB (2048MB) ya RAM.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Tecno Spark Plus K9 bei na Sifa zake

Kioo

Tecno R7 na Tecno D7 zote mbili zina skrini ya 5.5-inchi. D7 inakuja na pixels resolution saizi ya 480 x 854  wakati R7 ina pixels resolution saizi ya 720 x 1280. Matokeo ya hili ni kwamba Tecno R7 ina uwezo wa kuonyesha vizuri zaidi. Kioo cha Tecno R7 pia kimejengwa kwenye teknolojia ya IPS na ulinzi wa kioo wa Corning Gorilla.

Kamera

Kama unavyotarajia, Tecno R7 inakuja na kamera bora zaidi. Kamera ya megapixel 13 yenye autofocus na flash upande wa nyuma na megapixels 5 kamera ya mbele. Kwa kulinganisha, Tecno D7 ina kamera ya nyuma yenye megapixels  5 na kamera ya mbele yenye megapixel 2.

SOMA NA HII:  Nafasi za ajira serikalini sasa kuwafikia wahitimu kwa simu ya mkononi

Uhifadhi wa Ndani na Upanuzi

Tecno D7 inakuja na 4GB ya hifadhi ya ndani, wakati Tecno R7 inakuja na 16GB. Hii inamaanisha unaweza kupakia zaidi kwenye R7 yako kabla ya kuhitaji memori kadi kwajili ya upanuzi. Simu zote zinaweza kupanuliwa na memori kadi ya hadi 32GB.

Betri

Tecno D7 inakuja na betri ya 2500mAh, wakati Tecno R7 ina betri ya 2430mAh. Hii ni sehemu pekee ambapo Tecno D7 inaizidi R7. Hatuelewi kwa nini Tecno ilipunguza ukubwa wa betri ya R7.

Matokeo yake ni kwamba kwa kuzingatia screen resolution na uwezo wa prosesa wa Tecno R7, itakuwa na maisha mafupi ya betri kuliko D7.

SOMA NA HII:  Option ya Kubadili 'Storage' Kwenye Samsung J5

Unapaswa kununua ipi?

Tecno R7 inaizidi Tecno D7 katika vipengele vyote isipo kuwa upungufu mdogo katika maisha ya betri. Tecno R7 ni ndogo na nzuri zaidi. Uamuzi wa ununuzi hutegemea na bei. Sababu pekee ya kupendekeza D7 na sio R7 ni bei.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako