Hizi Hapa Ndio Simu Kumi Bora kwa Mwaka 2018


Mikutano ya CES na MWC kwa mwaka 2018 tayari imepita na simu mpya sasa zimefika mikononi mwa wanunuzi mwaka 2018. Kuna uwezekano wa kuwa simu mpya zaidi zitazinduliwa katika miezi ijayo, lakini ni wakati wa kufahamu simu bora zaidi mpaka sasa.

simu

Kumbuka list hii imepangwa kwa kuzingatia maoni mbalimbali ya watu kupitia tovuti mbalimbali, bila kusahau data za idadi ya mauzo ya simu husika. Basi baada ya kusema hayo basi moja kwa moja twende tukanze list hii.

1. Samsung Galaxy S9/S9 Plus

Samsung
Samsung

Samsung hivi karibuni ilizindua Galaxy S9 na S9 Plus na simu hizi tayari zimeingia sokoni wiki hii. Ni mageuzi katika matoleo ya Galaxy S, ni moja ya simu inayoongoza katika kuwa na ukamilifu unaotarajiwa kwenye simu janja za leo.

Ubora wa skrini ya Samsung unaendelea kuchukua nafasi katika kila tolea jipya, simu hii inashindana na simu ya Apple iPhone X. Ina 6GB ya RAM, processor ya Qualcomm Snapdragon 845 yenye kasi zaidi, kamera mbili za nyuma, uwezo wa kuongeza kadi zisizo na gharama za microSD, Bixby assitant imeimarishwa zaidi, teknolojia ya Samsung Pay payment, mfumo wa kuchaji kwa haraka pia unaweza kuchaji kwa njia ya wireless, IP68 dust na uwezo wa kuzuia maji, USB Type-C, na 3.5mm headset jack. Pia inakuja na mfumo wa Android 8.0 Oreo. Hakuna kitu kinachokosekana kwenye Galaxy S9 Plus na inastahili nafasi ya juu.

2. Apple iPhone X

Apple iPhone X sasa ipo mikononi mwa wanunuzi na inapatikana katika maduka mbalimbali. Ni simu janja ya bei kubwa zaidi kuwahi kuzindua kwa bei ya mwanzo ya dola 999 kwa 64GB na $ 1,149 kwa 256GB.

IPhone X ni ya kipekee kuwahi kubuni na iPhone tangu kutolewa kwa simu ya kwanza ya iPhone iliyozinduliwa miaka 10 iliyopita. Ina skrini kubwa ya 5.8-inch na bezels ndogo na hakuna kitufe cha nyumbani (home button). Samsung OLED panel imetumika kwa mara ya kwanza kwenye iPhone. Kuna kamera mbili kwa nyuma na njia mpya ya kutumia iPhone kutokana na kutokuwepo kwa kitufe cha nyumbani na power button ya kawaida.

The iPhone X is powered by the new A11 bionic chip and M11 motion coprocessor so it flies with iOS 11. It has an IP67 dust and water resistant rating. Glass is now used on the back to support wireless charging. The front facing camera is 7 megapixels and labeled TrueDepth so you can take portrait selfies.
IPhone X inakuja na A11 bionic chip mpya naM11 motion coprocessor inatumia mfumo wa iOS 11. Ina IP67 dust na uwezo wa kuzuia maji. Kamera ya mbele ina megapixels 7.

3. Samsung Galaxy Note 8

Galaxy Note 8 ilikuwa nafasi ya juu kwa muda wa miezi michache kwa sababu ilikuwa simu janja yenye uwezo mkubwa zaidi kwenye soko na inawezekana bado ipo nafasi ya juu. Galaxy S9 Plus ina maboresho machache, lakini hakuna S Pen, na iPhone X pia ni simu janja yenye uwezo mkubwa.

Soma Uchambuzi Kamili: Ifahamu simu ya Samsung Galaxy Note 8 bei na Sifa zake

Samsung Galaxy Note 8 ina sifa zote nzuri zinazopatikana katika S9 na S9 Plus, lakini bado haina Android 8 Oreo, inatumia processor ya Snapdragon 835, na kamera zake hazina “dual mechanical aperture”. Pia ina S Pen na ikiwa unapenda kutumia stylus kwenye simu yako basi Note 8 inakufaa.

4. Google Pixel 2 XL na Pixel 2

Google Pixel 2 na Pixel 2 XL huleta baadhi ya vipengele ambavyo nilikuwqa natamani kuviona (kuzuia maji na bezels ndogo kwenye XL) na nyingine ambazo sizitaki (kuondolewa kwa 3.5mm headset jack). Zote ni simu bora za Android hivyo kama unataka simu inayofanya kazi kwa kufata jinsi Google ilivyounda Android kufanya kazi basi Pixel 2 inaweza kuwa simu sahihi.

Google Pixel 2 XL ina skrini ya ukubwa wa 6-inch, processor ya Snapdragon 835, 4GB ya RAM, 64GB na 128GB ya uhifadhi, kamera moja ya nyuma ya megapixel 12, IP67 dust na uwezo wa kuzuia maji na betri ya 3520 mAh. Pixel 2 ndogo ina skrini ya inchi 5 na betri ndogo huku sifa zingine zikifanana na toleo la XL.

5. Apple iPhone 8/8 Plus

Apple iPhone 8/8 Plus mpya inaonekana kama iPhone 7/7 Plus, lakini ina uwezo wa kuchaji kwa njia ya wireless. Kwa kuongeza iPhones mpya ina processor iliyoboreshwa kidogo, kamera iliyoboreshwa, na Skrini bora ya LCD.

 

Kuna spika za stereo kwa ajiri ya utendaji mzuri wa sauti, lakini hakuna 3.5mm headphone jack. iPhone mpya ina uwezo wa kuchaji kwa haraka unaweza kupata hadi asilimia 50 ya uwezo wa betri ndani ya dakika 30.

Hakuna chaguo la uwezo wa 128GB, inapatikana katika matoleo yenye uhifadhi wa 64GB na 256GB.

6. Huawei Mate 10 Pro

Mate 10 Pro ina skrini ya ukubwa wa 6 inch, Kirin 970 processor iliyo naeural network processing unit, Android 8.0 Oreo na EMUI 8, 6 GB RAM, hifadhi ya ndani ya 128 GB, kamera mbili za nyuma, kamera ya mbele ya megapixel 8, na betri ya 4,000 mAh.

Kazi moja inayotofautisha Huawei Mate 10 Pro na Pixel 2, kwa biashara, ni uwezo wa kuunganisha kupitia USB Type-C port kwenye kompyuta, keyboard, na kipanya kupata uzoefu kamili wa desktop. Galaxy Note 8 na Galaxy S9 / S9 Plus zinaweza kufanya hivyo kwa njia ya kifaa cha DeX, lakini Mate 10 Pro haihitaji kifaa kingine kufanya kazi hii.

7. OnePlus 5T

OnePlus

Karibu miezi sita baada ya kuzinduliwa kwa OnePlus 5, tunaona uzinduzi wa OnePlus 5T ikiwa na ukubwa na maboresho ambayo yamefanya iwe simu janja nzuri. Bei yake ni, $ 499 na $ 559 (toleo la 128GB).

OnePlus 5T inakuja na RAM ya 6GB na hifadhi ya ndani ya 64GB kwa $ 499 tu. Tofauti na flagships nyingine kutoka Samsung na LG, OnePlus ina historia ya kutoa sasisho za mara kwa mara na pia jumuiya inayofanya kazi ya watumiaji na waendelezaji ili uweze kutumia muda wako kuifanya simu iwe unavyotaka.

8. Sony Xperia XZ2

Ni muda mrefu umepita tangu kwa simu ya Sony Xperia kuingia kwenye orodha yangu simu 10 nzuri zaidi, lakini baada ya kuhamishia fingerprint scanner  nyuma na kuimarisha ubunifu wao ni vigumu kuisahau simu ya Sony Xperia XZ2.

Sony Xperia XZ2 inakuja na Qualcomm Snapdragon 845 processor, Android 8.0 Oreo, 4GB ya RAM, 64GB ya hifadhi ya ndani na msaada wa kadi ya microSD, mfumo wa kuzuia maji na vumbi, skrini ya 5.7 inch na kamera ya nyuma ya megapixel 19.

Hatuna maelezo ya bei au upatikanaji wa simu hii mpya ya Sony.

9. LG V30/V30S

V30 inakuja na processor ya Qualcomm Snapdragon 835, 4GB ya RAM, 64GB ya hifadhi ya ndani na slot ya microSD, ina uwezo wa kuzuia vumbi na maji. Utapata kamera mbili za nyuma, moja ina megapixel ya 16 na nyingine megapixel 13,.

Katika MWC, LG ilionyesha V30S ambayo ina vipengele vya LG V30 Plus na baadhi ya maboresho ya ziada ya programu hasa kwa njia ya AI katika uzoefu wa kamera. Haijaingia sokoni bado na habari kuhusu bei yake bado hazijatolewa.

10. BlackBerry Motion

BlackBerry Motion ni toleo kamili la simu yenye skrini ya kugusa (touchscreen ) na ina vipengele vinavyofanana na BlackBerry KEYone. Ina 2GHz octa-core Qualcomm Snapdragon 625 chipset na 650MHz Adreno 506 GPU na 4GB ya RAM, Skrini ya ukubwa wa 5.5 inch 1920 x 1080, betri ya 4000 mAh kukupa maisha marefu ya betri, kamera ya nyuma yenye 12 na kamera ya mbele ya megapixel 8 kamera ya mbele, na sehemu ya kuweka memori kadi.

BlackBerry imejenga sifa kwa kutoa programu na sasisho za usalama kwa wakati, mara nyingi hutoa sasisho hizi siku chache baada ya Google kuzitoa kwenye Pixel. BlackBerry Hub pia ni chombo cha mawasiliano chenye ufanisi sana kukusaidia unapokuwa na tatizo.

One Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA