Sambaza:

Katika chapisho hili, tutaangalia au tutazingatia simu nzuri au bora na simu mpya zinazozalishwa na Tecno Mobile. Simu ambazo zimeorodheshwa katika chapisho hili zimechaguliwa kulingana na umaarufu wake, uwezo na maoni ya mtumiaji. Mpangilio huu wa Simu bora za Tecno umetokana na mtazamo wangu mwenyewe, unaweza kuwa na mtazamo tofauti, lakini nimejitahidi kadri iwezekanavyo kutokuwa na ubaguzi kwenye orodha. Tutaanzia kwenye simu zisizojulikana sana hadi kwenye simu maarufu zaidi au bora za Tecno. Kabla ya kuendelea tuzungumze kidogo kuhusu tecno mobile.

Tecno Mobile ni mojawapo ya kampuni kubwa ya kutengeneza simu janja barani Afrika na mabara mengine. Ni kampuni ya Kichina inayozalisha simu janja, tablets na feature phones. Lengo lao ni kuzalisha vifaa vyenye uwezo mkubwa (high-end devices) vinavyoweza kushindana au kuzizidi simu za mkononi kutoka kwa wazalishaji kama Samsung, Apple, Huawei na wengine. Simu zinazozalishwa na kampuni hii ni za bei nafuu au bei ya chini ikilinganishwa na washindani wao.

Simu za Tecnoza za Hivi Karibuni

Hii ni orodha ya simu za mkononi za Tecno zilizotoka hivi karibuni ikiwa ni pamoja na vipengele vyake vya msingi. Tumia kiungo cha “Bonyeza hapa” ili ufikie specs kamili, Bei na ukaguzi wa kila simu.

Tecno WX4

Sifa Muhimu za Tecno WX4

 • Mfumo wa Uendeshaji: Android 7.0 Nougat With HiOS
 • Ukubwa wa Kioo: 5.0 inches FWVGA screen. 720 x 1280 pixels (297 PPI)
 • Chipset: MediaTek
 • Uwezo wa Processor: Quad-core 1.3 GHz
 • Uwezo wa RAM: 1GB RAM
 • Ukubwa wa Ndani: 16GB
 • Ukubwa wa Nje: microSD, mpaka ukubwa wa 32GB
 • Kamera ya Nyuma : 8 MP na LED flash
 • Kamera ya Mbele: 8 MP na LED flash
 • Uwezo wa Mtandao: 3G
 • Uwezo wa Battery: 2800 mAh Battery

Angalia Uwezo na Bei ya Tecno WX4 hapa.

Tecno Wx4 Pro

Sifa Muhimu za Tecno Wx4 Pro

 • Ukubwa wa Kioo: 5.0-inch, 720 * 1280 pixels IPS HD
 • Kamera ya Mbele: 8.0 MP + LED flash
 • Kamera ya Nyuma: 8.0 MP + LED flash
 • Memori: 2GB RAM, 16 GB internal + SD support
 • Betri: 2800 mAh Non-removable
 • Mfumo wa Uendeshaji: Android 7.0 Nougat
 • Mtandao: 2G, 3G
 • Fingerprint : Ndio

Tecno Wx3 P

Sifa Muhimu za Tecno Wx3 P

 • Mfumo wa Uendeshaji: Android 7.0 Nougat
 • Ukubwa wa Kioo: 5.0-inch, 480 * 854 pixels
 • Uwezo wa Memori: 1GB RAM, 8 GB internal + SD support
 • Ukubwa wa Ndani: 8GB
 • Kamera ya Nyuma : 5.0 MP + LED flash
 • Kamera ya Mbele: 5.0 MP + LED flash
 • Uwezo wa Mtandao: 3G (3G na 4G kwenye WX3 LTE)
 • Fingerprint: Ndio
 • Uwezo wa Battery: 5000 mAh Non-removable

Angalia Uwezo na Bei ya Tecno WX3 P hapa.

Tecno I7

Sifa Muhimu za Tecno I7

 • Kioo: 5.5-inch, 720 * 1280 pixels IPS HD
 • Kamera ya Mbele: 16.0 MP + LED flash
 • Kamera ya Nyuma: 13.0 MP + LED flash
 • Memori: 4GB RAM, 32 GB internal + SD support
 • Betri: 4000 mAh Non-removable
 • Mfumo wa Uendeshaji: Android 7.0 Nougat
 • Mtandao: 2G, 3G, 4G
 • Fingerprint :Ndo
SOMA NA HII:  Simu za Lenovo Na Bei Zake Nchini Tanzania

Simu Bora za Tecno unazoweza kununua 2017

Namba 9: Tecno W5

Sifa Muhimu za Tecno W5

 • Idadi ya Laini: Inatumia laini mbili
 • Mfumo wa Uendeshaji: Android 6.0 Marshmallow
 • Kioo: 5.5 inches AMOLED Touchscreen
 • RAM: 1 GB
 • Hifadhi ya Ndani: 16 GB
 • Kamera ya Mbele: 5 MP na LED Flash
 • Kamera ya Nyuma: 13 MP dual LED Flash
 • Betri: 3000 mAh (ya moja kwa moja)
 • Usalama: Fingerprint Scanner

Kwa mtazamo wangu binafsi, Tecno W5 (pia kuna toleo la LITE) ni simu bora ya Tecno inayouzwa bei nafuu kwa watumiaji wanaozingatia bajeti. Simu hii ya bei nafuu inakuja na kamera ya ajabu ya 13MP nyuma na LED flash ambayo inatumika wakati wa kupiga picha kwenye giza. Ikiwa wewe ni aina ya watu wanaopenda selfie, MP 5 inafaa kwa mahitaji yako.

Namba 8: Tecno Camon C7

Sifa Muhimu za Tecno Camon C7

 • Mfumo wa Uendeshaji: HiOS (Android 5.1)
 • Uwezo wa Mtandao: 2G, 3G, 4G.
 • Ukubwa wa Kioo: Inchi 5.5 pamoja na kioo chenye teknolojia ya IPS.
 • Uwezo wa Processor: Quad-core
 • Uwezo wa RAM: 2GB
 • Ukubwa wa Ndani: 16 GB.
 • Ukubwa wa Nje: microSD, mpaka ukubwa wa 128GB
 • Kamera ya Nyuma:  13.0 MP AF
 • Kamera ya Mbele: 5.0 MP na Flash
 • Uwezo wa Battery: 3000 mAh huku ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia ya Li-Ion

Tecno Camon C7 ni mwanachama mwingine wa Tecno Camon C Series. Ina vitu vingi vinavyofanana na Tecno Camon C9 ikiwa ni pamoja na kamera ya megapixels 13 mbele na nyuma. Tecno Camon C7 pia ina kipengele cha Fingerprint sensor na Iris scanner.

Namba 7: Tecno Boom J8

Sifa Muhimu za Tecno Boom J8

 • Mfumo wa Uendeshaji: HiOS (Android 5.1)
 • Uwezo wa Mtandao: 2G, 3G, 4G.
 • Ukubwa wa Kioo: Inchi 5.5 pamoja na kioo chenye teknolojia ya IPS.
 • Uwezo wa Processor: Quad-core
 • Uwezo wa RAM: 2GB
 • Ukubwa wa Ndani: 16 GB.
 • Ukubwa wa Nje: microSD, mpaka ukubwa wa 128GB
 • Kamera ya Nyuma:  13.0 MP AF
 • Kamera ya Mbele: 5.0 MP na Flash
 • Uwezo wa Battery: 3000 mAh huku ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia ya Li-Ion

Tecno Boom J8 ni miongoni mwa simu za mkononi za Tecno kwajili ya muziki ina nguvu na gharama nafuu. Boom J8 inakuja na kioo cha HD inchi 5.5 na screen resolution ya 1280 x 720 pixels. Kwenye kamera, Boom J8 inajumuisha kamera ya nyuma ya mexapixels 13 na LED flash na kamera ya mbele ya megapixels 5.

Kwa kuwa na quad-core MediaTek MT6753 processor, unaweza kutarajia utendaji mzuri kutoka kwenye smartphone hii ya kiwango cha kati.

Ifahamu zaidi simu ya Tecno Boom J8 bei na Sifa zake hapa

Namba 6: Tecno Phantom 5

Sifa Muhimu za Tecno Phantom 5

 • Mfumo wa Uendeshaji: Android 5.1 Lollipop
 • Uwezo wa Mtandao: 2G, 3G, 4G.
 • Ukubwa wa Kioo: Inchi 5.5 pamoja na kioo chenye teknolojia ya IPS.
 • Screen Resolution: 1080 x 1920 pixels (400ppi)
 • Uwezo wa Processor: 64-bit, 1.5GHz Octa-core Processor (MediaTek MT6753)
 • Uwezo wa RAM: 3GB
 • Ukubwa wa Ndani: 32 GB.
 • Ukubwa wa Nje: microSD, mpaka ukubwa wa 128GB
 • Kamera ya Nyuma:  Megapixel 13
 • Kamera ya Mbele: Megapixel 8
 • Ulinzi: Fingerprint Sensor (Rear)
 • Uwezo wa Battery: 3000 mAh huku ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia ya Li-Ion
SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Tecno Phantom 6 Plus bei na Sifa zake

Tecno Phantom 5 ni mrithi wa Tecno Phantom Z, ikiwa na kioo cha HD chenye 5.5-inch, 3GB ya RAM, fingerprint sensor, 4G LTE ya haraka, na inakuja na Android 5.1 Lollipop. Ingawa toleo la Android limeboreshwa kuwa Android 6.0 Marshmallow.

Ifahamu zaidi simu ya Tecno Phantom 5 bei na Sifa zake hapa

 Namba 5: Tecno Camon C9

Sifa Muhimu za Tecno Camon C9

 • Mfumo wa Uendeshaji: Android 6.0 Marshmallow (HIOS V1.0)
 • Uwezo wa Mtandao: 2G, 3G, 4G.
 • Ukubwa wa Kioo: Inchi 5.5 pamoja na kioo chenye teknolojia ya IPS.
 • Uwezo wa Processor: Octa-core Processor
 • Uwezo wa RAM: 2GB
 • Ukubwa wa Ndani: 16 GB.
 • Ukubwa wa Nje: microSD, mpaka ukubwa wa 128GB
 • Kamera ya Nyuma:  13.0 MP AF
 • Kamera ya Mbele: Megapixel 13.0
 • Ulinzi: Sensor: G-sensor, Light Sensor, Proximity Sensor
 • Uwezo wa Battery: 3000 mAh huku ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia ya Li-Ion

Tecno Camon C9 ni kati ya simu za Tecno za bei nafuu ni simu janja ya android na mrithi wa Tecno Camon C8. Camon C9 ina kamera yenye ubora na processor yenye kasi zaidi kuliko Camon C8. Inakuja na Android 6.0 Marshmallow, 2GB RAM, na iris scanner.

Ifahamu zaidi simu ya Tecno Camon C9 bei na Sifa zake hapa

Namba 4: Tecno L9 Plus

Sifa za Tecno L9 Plus

 • Mfumo wa Uendeshaji: Android 7.0 (Nougat) with HiOS
 • Uwezo wa Mtandao: 2G, 3G.
 • Ukubwa wa Kioo: Inchi 6.0 pamoja na kioo chenye teknolojia ya IPS.
 • Screen Resolution: 720 x 1280 pixels (244ppi)
 • Uwezo wa Processor: 1.3GHz quad-core Mediatek
 • Uwezo wa RAM: 3GB
 • Ukubwa wa Ndani: 16 GB.
 • Ukubwa wa Nje: microSD, mpaka ukubwa wa 128GB
 • Kamera ya Nyuma:  Megapixel 13
 • Kamera ya Mbele: Megapixel 5
 • Ulinzi: Fingerprint Sensor
 • Uwezo wa Battery: 5000 mAh huku ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia ya Li-Ion

Tecno L9 Plus ni mrithi wa Tecno L8 Plus. Simu mpya ya Tecno inakuja na programu iliyoboreshwa na kioo kikubwa zaidi. Tecno L9 Plus ina kio cha IPS cha inchi 6.0, lakini kipengele maarufu zaidi ambacho Tecno wamekizungumzia ni kwamba L9 Plus inaweza kudumu na chaji hadi masaa 72 kwa betri ya 5000mAh.

Ifahamu zaidi simu ya Tecno L9 Plus bei na Sifa zake hapa

Namba 3: Tecno Phantom 6

Sifa Muhimu za Tecno Phantom 6

 • Idadi ya Laini: Inatumia laini mbili
 • Mfumo wa Uendeshaji: Android 6.0 (Marshmallow)
 • Kioo: 5.5 inches AMOLED Touchscreen
 • RAM: 3 GB
 • Hifadhi ya Ndani: 32 GB
 • Kamera ya Mbele: 8 MP na LED Flash
 • Kamera ya Nyuma: 18 MP na LED Flash
 • Betri: 2700 mAh (ya moja kwa moja)
 • Usalama: Iris Scanner
SOMA NA HII:  Unatumia "Lock ? " ya aina gani kwenye simu yako?

Ni Smartphone ya Mapinduzi imesaidia simu za Tecno kuingia ndani ya soko la simu za kiwango cha juu nchini Tanzania. Inapendeza, inakuja na kamera ya nyuma ya MP 18 wakati kamera ya mbele imechukua MP 8. Simu hii inaruhusu 4G LTE lakini kitu kizuri kwenye simu hii ni RAM ya 3 GB kwajili ya kufanya kazi nyingi, kucheza michezo ya HD na mengi zaidi.

Ifahamu zaidi simu ya Tecno Phantom 6 bei na Sifa zake hapa

Namba 2: Tecno Camon CX (AIR)

Sifa Muhimu za Tecno Camon CX (AIR)

 • Kamera: Nyuma– 13 MP / Mbele – 13 MP
 • Processor: 1.5 GHz Octa-core CPU
 • Mfumo wa Uendeshaji: Android v7.0 (Nougat)
 • RAM: 2 GB RAM
 • Uhifadhi wa ndani: 16 GB ROM
 • Betri: 3000 mAh
 • Sifa Zingine: Fingerprint sensor

Tecno Camon CX Air ni aina tofauti ya Camon CX. Ina ukubwa sawa na CX, lakini baadhi ya vipengele vimepunguzwa. Tecno Camon CX Air ni mojawapo ya simu za Tecno nyembamba zaidi ikiwa na 5.6mm tu. Pia imezingatia zaidi kamera kama simu nyingine za Tecno Camon ikiwa na kamera ya 13MP nyuma na mbele. Tecno Camon CX Air ina kioo cha 5.5-inch na resolution ya 720 x 1280.

Angalia Uwezo na Bei yake hapa.

Namba 1: Tecno phantom 6 Plus

Sifa za Tecno Phantom 6 Plus

 • Mfumo wa Uendeshaji: Android 6.0 Marshmallow with HiOS v1.0
 • Uwezo wa Mtandao: 2G, 3G, 4G.
 • Ukubwa wa Kioo: Inchi 5.95 pamoja na kioo chenye teknolojia ya IPS.
 • Screen Resolution: 1920 x 1080 pixels
 • Uwezo wa Processor: 2.1GHz Deca-core MediaTek Helio X20 Processor
 • Uwezo wa RAM: 4GB
 • Ukubwa wa Ndani: 64GB.
 • Ukubwa wa Nje: microSD, mpaka ukubwa wa 128GB
 • Kamera ya Nyuma: Ziko mbili zikiwa na Megapixel 21 zote zikiwa na teknolojia ya LED flash, Autofocus & 1080p@30fps video recording.
 • Kamera ya Mbele: Megapixel 8
 • Ulinzi: Accelerometer, Iris scanner, Proximity Sensor & Fingerprint Sensor.
 • Uwezo wa Battery: 4,050 mAh huku ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia ya Li-Ion

Tecno Phantom 6 Plus ilitoka mwaka jana, na ni moja ya simu chache za kisasa zaidi kutoka Tecno .Tecno Phantom 6 Plus ni toleo la Tecno Phantom 6 lililo boreshwa zaidi . Simu imeshangaza wengi tofauti na ndugu yake, Phantom 6 kwa uwezo na sifa nyingi zaidi.

Ifahamu zaidi simu ya Tecno Phantom 6 Plus bei na Sifa zake hapa

Hizi ni simu bora ambazo tecno imewahi kutengeneza, zina uwezo mkubwa na vipengele vingi na ndio sababu simu hizi zimekuwa bora kuliko zingine.

Thats it for the top 9 best tecno phones that is worth considering in 2017. Feel free to air your own view about this phone in the comment section and share if you like this post.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako