Simu Bora za Android Zinazouzwa Chini ya Tsh 400,000


Utastaajabu kujua kwamba wakati mwingine unaweza kupata simu nzuri za Android ambazo zina uwezo mkubwa kama flaships maaraufu duniani kwa bei nafuu kutoka kwa brands nyingine. Ikiwa hutuamini, basi unapaswa kuangalia orodha hii ya simu bora zaidi zinazouzwa kwa bei chini ya Tsh 400,000. Usisahau kutuambia ni simu gani imekuvutia kati ya hizi kwa kutoa maoni yako mwishoni mwa chapisho.

1: Infinix Hot 5 Lite (X559)

Infinix sio brand mpya inayohitaji kujitambulisha. Kitu kinachotakiwa kutambulishwa ni simu yao yenye uwezo mkubwa Hot 5 Lite (X559). Ina inchi 5.5 ya skrini na resolution ya 1280 x 720p. Simu hii inakuja na  quad-core 1GB CPU ambayo ina kasi ya 1.3GHz.

Simu janja inakuja na hifadhi ya ndani ya ukubwa wa 16GB ambayo inaweza kupanuliwa hadi 32GB.

Katika sehemu ya kamera, Infinix anafanya vizuri kwa kuleta shooter ya 8MP nyuma na 5MP mbele. Inatumia mfumo wa Android 7 Nougat, kipengele kikubwa zaidi cha simu hii kwa watumiaji wengi (na soko la Tanzania) ni betri yake kubwa ya 4000mAh.

2: Tecno K8

Inajulikana kwa wengine kama Tecno Spark Pro, K8 ni simu yenye inchi 5.5 ya skrini ya HD (1280 x 720). Tukiangalia uwezo wake, moja ya kitu ambacho kina haki ya kupata maelezo ya ziada ni kamera zake, kamera ya nyuma ina 13MP na kamera ya mbele ni 8MP. Inakuja na quad-core,1.25GHz CPU na RAM ya 1GB. Hifadhi ya ndani ni 16GB ambayo inaweza kupanuliwa hadi 32GB.

Pia ina fingerprint sensor na betri nzuri ya 3000mAh inatumia mfumo wa Android 7 Nougat.

3: Tecno Camon CM

Simu ya Tecno Camon CM ni ongezeko la hivi karibuni kwenye mfululizo wa simu za TECNO zilizowekeza zaidi upande wa kamera pia ni mrithi wa simu maarufu ya Camon Cx . Hii ni smartphone ya kwanza ya TECNO kuja na bezel-less, kwa uwiano wa 18: 9 , mfumo ambao ulikua maarufu sana kwenye simu janja mwaka wa 2017.

Camon CM inakuja na kioo chenye inchi 5.7, corning gorilla glass 3 protection , Quad-core MediaTek chipset , 2GB RAM , uhifadhi wa ndani wa 16GBna betri yenye uwezo wa 3000mAh. Simu ya CM inakuja na kamera yenye 13MP mbele na nyuma ikiwa na LED flash na f/2.0 lens.

4: Motorola Moto E4


Motorola Moto E4 ni simu janja ya Android iliyozinduliwa Juni 2017. Ina skrini ya ukubwa wa inchi  5.0 na resolution ya 720*1280 pixels. Motorola Moto E4 inatumia 1.3GHz quad-core MediaTek MTK6737M processor na inakuja na RAM ya 2GB.

Simu janja hii ina hifadhi ya ndani ya 16GB pia unaweza kuweka microSD card hadi ya 32GB .

Kwa kuwa siku hizi kamera zinahusika sana, Motorola Moto E4 inakuja na kamera ya nyuma ya megapixel ya 8 na kamera ya mbele ya 5 MP. Simu hii ina betri yenye ujazo wa 2800 mAh na pia inakuja na Corning Gorilla Glass 3.

5: Nokia 3

Nokia 3 ilizinduliwa mwezi Februari 2017. Simu inakuja na skrini ya 5.00-inch kwa resolution of 720*280 pixels. Bei ya Nokia 3 nchini Tanzania ni kati ya 300,000 – 350,000.

Nokia 3 inatumia 1.3GHz quad-core MediaTek 6737 processor na inakuja na 2GB ya RAM. Simu hii ina 16GB ya hifadhi ya ndani ambayo inaweza kupanuliwa hadi 128GB kupitia kadi ya microSD. Nokia 3 ina kamera ya nyuma ya 8-megapixel na kamera ya mbele ina  8-megapixel.

Nokia 3 inatumia Android 7.0 na ina betri yenye ujazo wa 2630mAh .

6: Oppo A37

Oppo A37 ilizinduliwa mwezi wa Juni 2016. Simu inakuja na skrini ya 5.00-inchi na resolution ya 720*1280 pixels kwenye PPI ya saizi 293 kwa inchi. Bei ya simu ya Oppo A37 bei nchini Tanzania huanza Tsh 340.000.

Oppo A37 inatumia 1.2GHz quad-core Qualcomm Snapdragon 410 processor na inakuja na 2GB ya RAM. Simu hii ina 16GB ya hifadhi ya ndani ambayo inaweza kupanuliwa hadi 128GB kupitia kadi ya microSD. Oppo A37 inakuja na kamera ya nyuma ya megapixel 8 na kamera ya mbele ya megapixel ya 5 kwa ajili ya selfies.

Oppo A37 inatumia Android 5.1 na ina  betri isiyoweza kutolewa ya 2630mAh.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA