Home Nyingine Shirika la ndege la Malawi kufanya safari ya ndege itakayosimamiwa na wanawake tu kutoka Malawi hadi Tanzania

Shirika la ndege la Malawi kufanya safari ya ndege itakayosimamiwa na wanawake tu kutoka Malawi hadi Tanzania

0
0

Shirika la ndege la Malawi litaweka historia baada ya kutangaza kwamba linapanga kufanya safari ya ndege itakayosimamiwa na marubani na wasaidizi wa abiria wanawake pekee, ndege itaruka kutoka mji wa Blantyre hadi Dar-es-Salaam nchini Tanzania.

Safari hiyo, inatarajiwa kufanyika Alhamisi wiki hii 16/3/2017, ndege itatua kwa muda Lilongwe kabla ya kuelekea Dar . Tukio hilo litakuwa la kuhistoria kwasababu itakuwa ni mara ya kwanza kuandaliwa na shirika hilo.

Taarifa kutoka kwa shirika hilo la ndege, lilisema lengo ni kufanikisha ulimwengu ambao “unakumbatia jinsia zote”.

Ndege hiyo itakuwa chini ya Kapteni Yolanda Kaunda akisaidiwa na Lusekelo Mwenifumbo,24,alisomea taaluma ya uchukuzi wa ndege mjini Addis Ababa, Ethiopia.

“Lengo la hatua hii ni kuwahamasisha wasichana ambao wangependa kufanya kazi katika uchukuzi wa ndege lakini kwa njia moja au nyingine hufikiria ni vigumu au kwamba ni kazi ambayo wanawake hawaiwezi,” taarifa ya Malawi Airlines ilisema.

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *