Nyingine

Shamsa Ford amepokea kichapo na kupasuka uso

Msanii wa filamu Shamsa Ford amepigwa Jumanne hii katika harakati za kuamlia ugomvi wa watu ambao haijajulikana moja kwa moja ni nani, na sababu za ugomvi wao ni nini.

Muigizaji huyo amedai alipigwa ngumi ya uso katika harakati za kutafuta usalama wa watu hao ambao walikuwa wakipigana.

“Jana kwa moyo mmoja nimeenda kuamlia ugomvi watu wasipigane mwisho wa siku nikaambulia Mimi ngumi..HUYU mtu alishiba sana aiseee ngumi ilikuwa nzito sana..😃😃 niombeeni ndugu zangu panauma,” aliandika Shamsa Instagram.

Kwa sasa muigizaji anaendelea na matibabu.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *