Nyingine

Serikali yatoa sababu za Watanzania kufukuzwa Msumbiji

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema kuwa Watanzania waliokuwa nchini Msumbiji wamefukuzwa kutokana na kukiuka taratibu na sheria za kuishi nchini humo.

Mahiga amesema kuwa Watanzania hao wamefukuzwa Msumbiji baada ya kubainika kuwa wanaishi nchini humo bila vibali vya kuishi, na kutofuata vigezo walivyokuwa wamepewa na mamlaka husika ya nchi hiyo.

Hayo ameyasema wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ugeni unaotarajiwa kuwepo nchini Tanzania wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni anayetarajiwa kufanya ziara ya siku mbili ya Kitaifa nchini Februari 25 na 26, 2017.

Rais wa Visiwa va Shelisheli, Danny Faure naye atawasili Tanzania kwa ziara ya siku mbili kuanzia Tarehe 27-28, februari mwaka huu

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close