Sambaza:

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene

Serikali imesema jumla ya walimu 3,081 wameajiriwa, hivyo bado kuna nafasi ya walimu 1,048 kati ya nafasi 4,129 za walimu wa Sayansi na Hisabati zilizotolewa kibali cha ajira.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene na kuwataka walimu wote walioajiriwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kuanzia tarehe 18 hadi 25 mwezi huu.

Amesema walimu walioajiriwa wamepangwa moja kwa moja na TAMISEMI katika halmashauri zote nchini ambazo zina upugufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati.

SOMA NA HII:  Kenya yatengeneza satelaiti yake kurushwa anga za juu Machi mwaka huu

Simbachawene ameongeza kuwa kati ya walimu hao walioajairiwa, walimu 1,537 ni wa Shahada na walimu 1,544 ni wa Stashahada.

“Sehemu kubwa ya walimu wa Shahada wamepangwa kwenye shule za kidato cha tano na sita na wachache kwenye shule za kidato cha kwanza hadi cha nne’’ amesema.

Aidha, amekiri kuwa kuna upungufu wa walimu 26,026 wa masomo Sayansi na Hisabati katika shule mbalimbali za sekondari nchini.

“Moja ya changamoto kubwa ambazo zinaikabili sekta ndogo ya elimu ya sekondari ni upungufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati ambapo upungufu uliopo katika shule 3,602 ni walimu 26,026 sawa na asilimia 60.14 ya walimu 43,248 wanaohitajika,” amesema Simbachawene

Amesema walimu wanaohitajika kwa masomo hayo ni walimu 43,248 lakini waliopo kwa sasa ni 17,252 pekee.

SOMA NA HII:  Orodha ya Maneno ya Teknolojia na Tafsiri zake kwa Kiswahili

 

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako