Serikali yaagiza Polisi kumuachia Nay wa mitego na kuruhusu wimbo wa ‘Wapo’Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo Dr. Harrison Mwakyembe ameagiza Polisi nchini kumuachia msanii wa Bongofleva Nay wa Mitego aliyekuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutoa wimbo usio na maadili, Waziri Mwakyembe amesema Rais ameshauri wimbo wa ‘WAPO’ auboreshe kwa kutaja na wakwepa kodi.

Waziri Mwakyembe ameishauri pia BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo huo na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.

Akiongea na Wandishi wa Habari muda huu mjini Dodoma, Dk. Mwakyembe amesema hata Rais Magufuli amefurahishwa na wimbo huo wa WAPO na kumshauri Msanii huyo kama inawezekana aendelee kutaja watu wengine kama vile Wakwepa Kodi, Wauza Unga, Wabwia Unga, Wezi pamoja na watu wengine wasio na maadili mema katika jamii.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA