Seneta Marekani mashakani kwa kudhalilisha Kiswahili katika mahojiano na Mmiliki wa Facebook


Seneta John Kennedy wa chama tawala cha Republican kutoka jimbo la Louisiana nchini Marekani amekosolewa na watumizi wa mitandao ya kijamii kutokana na hatua yake ya kuonekana kuikejeli na kuidhalilisha lugha ya Kiswahili.

Katika tamko lake Seneta John Kennedy jana alimtaka Mkurugenzi wa Mtandao wa Kijamii cha Facebook Mark Zuckerberg kutumia Kiingereza na si Kiswahili katika kuandika mapatano baina ya mtandao wa kijamii wa Facebook na wanaoutumia.

Seneta Kennedy alikuwa kimhoji Zuckerbeg kuhusu mapatano baina ya Facebook na watumizi wa mtandao huo na kusema ni magumu sana kwa Mmarekani wa kawaida kuelewa.

Alimtaka Zuckerberg aamuru mawakili wake wasiandike mapatano kwa Kiswahili bali kwa lugha ambayo kila mtu anaifahamu. “Nataka uende uamuru mawakili wako unaowalipa dola 1,200 kwa saa, kuandika kwa Kiingereza na si kwa Kiswahili, ili kila Mmarekani aelewe”.

Wazungumzaji lugha ya Kiswahili na watumiaji wengine wa mitandao ya Kijamii wamesema Seneta huyo wa chama Rais Donald Trump alikuwa na nia ya kuwakejeli watumizi wa Kiswahili. Alipohojiwa na CNN na kuulizwa iwapo ataomba msamaha baada ya tamko lake kuwakasirisha wengi, Seneta Kennedy amesema, “Siombi msamaha, nadhani kila mtu alifahamu kusudio langu.”

Mtumizi wa Twitter aliyejitambulisha kama F Crouter aliandika hivi: “Sasa Seneta Kennedy anaikejeli lugha ya Kiswahili kama ambayo hakuna mtu anaifahamu. Afahamu kuwa mamilioni ya Waafirka wanazungumza lugha hii.”

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA