Habari za Teknolojia

Satelaiti ya kwanza ya Ghana sasa inafanya kazi

Satelaiti ya kwanza ya Ghana ilizinduliwa hivi karibuni katika obiti (orbit) sasa inafanya kazi, Kwa mujibu wa ripoti za TechCrunch.

Satelaiti ya kwanza ya Ghana sasa inafanya kazi

Kifaa hicho ni cubesat, “miniature satellite” ambayo ina uzito wa 1.33kg. GhanaSat-1 cubesat ilirushwa kwenye roketi ya SpaceX mwezi Julai na imeshafika katika obiti.

Akizungumza na TechCrunch, profesa wa Ghana Richard Damoah alisema satellite ina majukumu mawili.

“Ina kamera ambayo kazi yake ni ufuatiliaji wa kina wa pwani za Ghana,” alisema Damoah.

“Kisha kuna kipande cha elimu – tunataka kuitumia kuunganisha teknolojia ya satelaiti katika mtaala wa shule za sekondari.”

Satelaiti ilijengwa na timu ya wahandisi katika Chuo cha All Nations University na itasambaza habari kwenye kituo cha chini katika Chuo Kikuu cha Space Systems and Technology Laboratory.

Please subscribe to our newsletter

SOMA NA HII:  Japheth Kaluyu: Nayafahamu vyema zaidi matatizo ya Wakenya

Zinazohusiana

JIUNGE NA MAZUNGUMZO, TOA MAONI YAKO HAPA

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Lako