Habari za Teknolojia

Sasa unaweza kwenda Ethiopia wamezindua huduma ya e-visa mtandaoni kwajili ya wageni

Nchi ya pili Afrika kwa kuwa na wakazi wengi, Ethiopia imetangaza uzinduzi wa huduma ya mtandaoni ya visa ikiwa ni jitihada za kutengeneza njia rahisi zaidi kwa wageni wa kimataifa kuingia nchini humo.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari maendeleo ya mpango huo yalitangazwa, wageni wa kimataifa wanaweza kufikia huduma ya mtandaoni kwenye ukurasa mmoja wa Wavuti ambapo wanaweza kuomba, kulipa na kuhakikisha wanapata visa zao mtandaoni.

Mara baada ya maombi ya mtandaoni kuidhinishwa, waombaji watapata barua pepe itakayo wawezesha kusafiri hadi Ethiopia. Pasipoti zao zitaunganishwa na visa mara moja watakapofika Addis Ababa, mji mkuu wa nchi hiyo.

Huduma hiyo ilizinduliwa na Idara kuu ya Uhamiaji na Ustawi wa Ethiopia kwa kushirikiana na shirika la ndenge linalokua kwa kasi barani Afrika, Ethiopia Airlines.

“Ethiopia, the oldest independent civilization in Africa and one of the oldest in the world, is endowed with historical places, natural beauty, colourful and diverse cultural activities and various endemic wild animals which are of great interest to international tourists. However; we have not made best use of these natural resources to attract large number of tourists,” alisema Bw. Tewolde GebreMariam, Mkurugenzi Mtendaji wa Ethiopian Airlines.

Aliongeza, “To this effect, this project is part of a new national initiative to transform the tourism sector in the country. The full commencement of the Online Visa application and issuance system will promote tourism, trade and investment to the country. It will save time, energy and cost for travelers to Ethiopia in addition to the simplicity and convenience that it facilitates.”

Huduma mpya ya e-visa ilianza kufanya  kazi tarehe 12 Juni 2017. Je! Utatembelea Ethiopia unaweza kubonyeza hapa ili kujua zaidi kuhusu huduma.

SOMA NA HII:  Goal Technology kuanza kutumika kwa mara ya kwanza Afrika

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako