Sasa unaweza kutumia huduma za Uber kwenye app ya BBM


BBM

Creative Media Works, inayofanya kazi kama BBM Messenger, imeungana na Uber kuanzisha huduma ya Uber ndani ya app ya BBM.

Huduma hiyo inapatikana kwenye matoleo ya Android na iOS ya BBM na inaruhusu watumiaji kuagiza usafari wa Uber bila kutoka kwenye app hiyo.

Watumiaji wanaweza kufikia huduma ya Uber kupitia orodha ya BBM Discover na haihitaji kuwa na app ya Uber kwenye kifaa chako.

Itakapo funguka ndani ya programu ya BBM, Uber itahitaji wasafiri kuingia (sign in) kwa kutumia namba ya simu au akaunti ya mtandao wa kijamii.

Programu inatumia jukwaa la m.uber ili kuunganisha huduma ya Uber kwenye BBM.

m.uber ni mfumo wa mtandao unaopatikana duniani kote ambao hutoa uzoefu wa programu ya Uber bila kujali mahali, kasi ya mtandao, au kifaa.

 

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA