Download

Sasa Unaweza Install Samsung Browser Kwenye Simu Isiyo Ya Samsung

Samsung wana browser nzuri, kubaliana na hilo! Samsung browser, kwa mtazamo wangu, ni moja kati ya “browsers” za Android bora zaidi. Chukua neno langu, inafanya kazi kwa haraka, rahisi kutumia, inaruhusu upanuzi na programu za kuzuia matangazo.

Kwa kusema hayo, watu kutoka Samsung kwa wema wa mioyo yao wameamua kuruhusu wengine kufurahia matumizi ya kivinjari chao kwa kuiwezesha kufanya kazi kwenye simu ambazo sio za Samsung.

Nimeweza ku-install kwenye simu yangu ya Halotel 5510  kwa kutumia link hii kutoka APKMirror.

Kwa wale ambao bado wanahitaji “Google sync na Chrome”, usiwe na wasiwasi, unaweza kushusha “Chrome desktop extension” kwajiri ya ku-sync bookmarks.

Vitu vingine ni pamoja na “integrated QR code reader” kama ile ya Chrome, na “Physical Web support”, uwezo wa kutazama video za digrii 360 bila ya kifaa cha VR, uwezo wa moja kwa moja wa kulinganisha bei Amazon wakati unafanya manunuzi mtandaoni, na mengineyo.

Inavutia?

SOMA NA HII:  Option ya Kubadili 'Storage' Kwenye Samsung J5
Mada zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako