Simu

Samsung Wanataka kuifanya Galaxy Note kuwa “Gr3at Again”.

Ndio, Gr3at!

Kwa mujibu wa Evan Blass, “Samsung codename” kwajili ya Galaxy Note 8 ni “Samsung Gr3at.” Na hii imefanya nifikirie, kwa nini “3” na sio “e”?

Labda Samsung wanataka kuongeza vitu 3 ambavyo havijawahi kuwemo kwenye simu za Galaxy Note 8.

Pia inawezekana kwamba 3 inahusu “3x Optical Zoom” ambayo imekuwa ikizungumziwa siku za karibuni.

Njia yoyote utakayo chagua kuiangalia, Samsung wapo kwenye shinikizo kubwa sana kuhakikisha wanatoa kifaa bora zaidi kuliko mfululizo wa Galaxy S8.

Kwa sasa, kumekuwa na uvumi kwamba Galaxy Note 8 inaweza kuja na screen yenye 6.3-inch, Snapdragon 836 na kamera mbili.

Bila shaka, tunatakiwa kusubiri hadi Septemba kujua kuhusu simu hii (bila shaka), lakini mpaka sasa, unafikiria nini kuhusu codename hiyo?

SOMA NA HII:  Simu Mpya za Google Pixel 2 Zimevuja Kabla ya Kutoka (Bei+ Picha)
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

JIUNGE NA MAZUNGUMZO, TOA MAONI YAKO HAPA

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Lako