Sambaza:

Apple ya Google ni Galaxy Series. Kila mwaka, Samsung wanatoa simu mpya kuendeleza mfululizo huo, simu ambazo mara nyingi zinafanya vizuri zaidi sokoni kuliko simu nyingine za Android.

Wakati Samsung Galaxy S8 na S8 Plus zinatolewa, habari ya kuzinduliwa kwake ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii.

Kama ilivyotarajiwa, simu mpya ya Samsung ina vipengele ambavyo vilitabiliwa na vyanzo mbalimbali vya habari.

Kama wengi wenu mnavyojua,mfululizo wa simu za Galaxy siku zote zinakuwa daraja la kwanza linapokuja suala la kuendeleza “Flagship” ya simu zao.

Kioo kisicho na ukomo,muundo wake, kamera ya ajabu, kuingiza charge kwa haraka, ufanyi kazi wa haraka na waterproofness yake inafanya S8 kuwa mjadala ya jiji.

Na si ajabu kila shabiki wa Smartphone anataka kuwa na simu hii.

Simu za Galaxy daima zimekuwa zikitumika kama kiwango bora cha Android kinacho linganishwa na iphone.

Galaxy S8 imejengwa kutokana na historia ya Samsung kuendeleza ubunifu wa umbo zuri ajabu wa chombo chenye uwezo. Inapatikana kwa ukubwa wa inchi 5.8 Galaxy S8 na inchi 6.2 Galaxy S8+, yenye kioo kinachong’ara bila ukomo na umbo lake laini ambalo halina mikwaruzo, na vifungo au pembe kali. Matokeo ya teknlojia hii yaweza kuangalia bila vikwazo na kufanya shughuli nyingi kwa ufanisi zaidi.

Galaxy S8 ina kamera ya kiwango cha juu inayoweza kuona picha kwenye mwanga mdogo na kuondoa ukungu kwenye picha. Galaxy S8 inapiga picha zenye mng’aro mzuri hata kwenye mazingira ambayo si rafiki kwa upigaji picha. Ina kifaa kinachochuja picha chenyewe na flemu nyingi za kutayarishia picha, watumiaji watafurahia picha bora za kiwango cha juu. .

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Itel S12 bei na Sifa zake

Kamera ya mbele ina uwezo wa 8MP F1.7 autofocus na teknolojia ya kutambua uso kuhakikisha kuwa picha inayopigwa kutoka umbali wowote inalengwa na kuonekana vizuri. Galaxy S8 imewekewa kifaa cha hali ya juu 12MP F1.7 kamera ya nyuma. Teknolojia ya dual-pixel sensor, yenye uwazi mpana na uwezo wa kulenga yenyewe vyote vinafanya kazi kwa pamoja ili kutoa picha safi na nzuri hata kwenye maeneo yenye mwanga mdogo.

Sifa za Samsung Galaxy S8

Angalia vipengele vyote unavyotakiwa kuvijua kuhusu Galaxy S8.

 • SIM Type: Single SIM (Nano-SIM)/ Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by)
 • 3G Network: HSDPA 850 / 900 / 1700(AWS) / 1900 / 2100
 • 4G Network: LTE band 1(2100), 2(1900), 3(1800), 4(1700/2100), 5(850), 7(2600), 8(900), 17(700), 20(800), 28(700)
 • Operating System: Android 7.0 Nougat & Grace UX (Samsung customized skin)
 • Back Camera:  12 MP, f/1.7, 26mm, OIS, LED flash, phase detection autofocus
 • Front Camera: 8 MP, f/1.7, dual video call, Auto HDR, autofocus, 1440p@30fps,
 • Camera Features: 1/2.5″ sensor size, 1.4 µm pixel size, geo-tagging, simultaneous 4K video and 9MP image recording, touch focus, face/smile detection, Auto HDR, panorama
 • Display: 5.8 inches AMOLED display (~83.6% screen-to-body ratio) , 1440 x 2960 pixels (~570 ppi pixel density)
 • Screen:  Corning Gorilla Glass 5
 • Dimension Size: 148.9 x 68.1 x 8 mm (5.86 x 2.68 x 0.31 in)
 • Rear Build: Corning Gorilla Glass 5 back panel
 • Smartphone Weight: 155 g
 • Colours: Midnight Black, Coral ‘s Blue, Maple Gold Orchid Gray, Arctic Silver,
 • Processor Type: Qualcomm MSM8998 Snapdragon 835 & Octa-core (4×2.35 GHz Kryo & 4×1.9 GHz Kryo)
 • Graphics Processor: Adreno 540
 • RAM: 4 GB
 • Internal Storage: 64 GB
 • External Storage: microSD, Expandable to 256 GB (dedicated slot) – also comes with a single-SIM          model that is Expandableto 256 GB
 • Video Recording: 2160p@30fps, 1080p@60fps, HDR, dual-video rec.
 • USB Type: v3.1, Type-C 1.0 reversible connector
 • NFC: Yes
 • Bluetooth : v5.0, A2DP, LE, aptX
 • Security: Fingerprint , Iris Scanner
 • Sensors : Iris scanner, fingerprint (behind the phone) accelerometer, gyro, proximity, compass,                           barometer, heart rate, SpO2
 • Battery: 3000mAh (non-removable) also utilize wireless charging
SOMA NA HII:  Simujanja Unlocked: Maana ya Processor na Kazi Yake Kwenye Simu

Sifa za Galaxy S8 Plus

samsung s8 plus

Galaxy S8 inatofautiana kidogo na S8+, angalia sifa zake hapa chini kujua utofauti.

 • SIM Type: Single SIM (Nano-SIM)/ Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by)
 • 3G Network: HSDPA 850 / 900 / 1700(AWS) / 1900 / 2100
 • 4G Network: LTE band 1(2100), 2(1900), 3(1800), 4(1700/2100), 5(850), 7(2600), 8(900), 17(700), 20(800), 28(700)
 • Operating System: Android 7.0 Nougat & Grace UX (Samsung customized skin)
 • Back Camera:  12 MP, f/1.7, 26mm, OIS, LED flash, phase detection autofocus
 • Front Camera: 8 MP, f/1.7, dual video call, Auto HDR, autofocus, 1440p@30fps,
 • Camera Features: 1/2.5″ sensor size, 1.4 µm pixel size, geo-tagging, simultaneous 4K video and 9MP image recording, touch focus, face/smile detection, Auto HDR, panorama
 • Display: 5.8 inches AMOLED display (~83.6% screen-to-body ratio) , 1440 x 2960 pixels (~570 ppi pixel density)
 • Screen: Corning Gorilla Glass 5
 • Dimension Size: 159.5 x 73.4 x 8.1 mm (6.28 x 2.89 x 0.32 in)
 • Smartphone Weight: 173 g
 • Colours: Midnight Black, Coral ‘s Blue, Maple Gold Orchid Gray, Arctic Silver
 • Processor Type: Qualcomm MSM8998 Snapdragon 835 – Octa-core (4×2.35 GHz Kryo & 4×1.9 GHz Kryo)    Graphics Processor: Adreno 450
 • RAM: 4 GB
 • Internal Storage: 64 GB
 • External Storage: microSD, Expandable to 256 GB (dedicated slot) – also comes with a single-SIM  model that is Expandableto 256 GB
 • Video Recording: 2160p@30fps, 1080p@60fps, HDR, dual-video rec.
 • USB Type: v3.1, Type-C 1.0 reversible connector
 • NFC: Yes
 • Bluetooth : v5.0, A2DP, LE, aptX
 • Security: Fingerprint , Iris Scanner
 • Battery: 3500mAh ( (non-removable) also utilize wireless charging
SOMA NA HII:  Hizi Ndio Simu 4 Bora kwa Wapenzi wa Muziki

Galaxy S8 inakuja na vifaa vya msingi vya Galaxy ambavyo watu wanavipenda sana, hii ni pamoja na: IP68, microSD inaweza kupokea 256GB, inawaka wakati wote na kuonesha haraka pamoja na uwezo wa kuchaji bila kutumia waya.

Angalia video hii kujua zaidi juu ya Galaxy S8 na S8 +

Galaxy S8 inapatikana kwa bei ya rejareja iliyopendekezwa ya Tsh1,770,000 wakati Galaxy S8+ inauzwa kwa Tsh1,995,000. Watumiaji wataweza kuchagua kati ya rangi tatu kwa aina zote mbili za simu hizo, ambazo ni rangi nyeusi ambayo haijakolea sana , Orchid Grey, and Maple Gold.

Hatimaye, simu iliyotarajiwa na wengi ipo mbele yako. Kutokana na sifa zake hapo juu, je, S8 & S8+ zimefikia kiwango unachotaka, au kipo chini?

Shukrani kwa kusoma uchambuzi wa Galaxy S8, bei yake & vipengele . Ni matumaini yangu umefurahi ?

Unaweza kutumia kitufe hapa chini kumshirikisha rafiki yako uchambuzi huu wa kuvutia !


Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako