Nyingine

Samatta hakamatiki kazidi kuwa mtamu Ulaya

Baada ya kufunga magoli mawili kwenye mchezo wa Europa League wakati Genk ilipocheza ugenini dhidi ya Gent.

Leo March 12, 2017 nahodha huyo wa Taifa Stars amefanikiwa kufunga goli moja katika ushindi wa mabao 4-0 walioupata Genk wakiwa ugenini dhidi ya KVC Westerlo katika game hiyo Genk walifanikiwa kupata ushindi wa goli 4-o Mbwana Samatta akifunga goli la kwanza dakika ya 7.

Magoli mengine ya KRC Genk yalifungwa na Thomas Buffel dakika ya 27, Omar Colley dakika ya 62 na Malinovsky dakika ya 90.

Ushindi huo unaifanya Genk ifikishe jumla ya pointi 48 ikiwa katika nafasi ya nane (8) kwenye msimamo wa ligi ya Ubelgiji inayoshirikisha timu 16.

Mpaka sasa Samatta ndani ya mwezi March amefanikiwa kufunga jumla ya magoli matano yakiwemo mawili aliyofunga Alhamisi iliyopita katika michuano ya kombe la Europa League.

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close