Nyingine

Salamu za rambirambi kutoka kwa Rais Magufuli kufuatia vifo vya wanafunzi 32 Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa, taarifa ya vifo vya wanafunzi 32 wa darasa la saba, walimu 2 na dereva wagari la shule ya msingi iitwayo Lucky Vicent ya Arusha vilivyotokea leo saa 3 asubuhi baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika eneo Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

Wanafunzi na walimu hao walikuwa wakitoka shuleni kwao kwenda shule ya msingi iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mtihani wa ujirani mwema na walipofika katika eneo la Rhotia Marera basi walilopanda liliacha njia na kisha kutumbukia korongoni ambako limesababisha vifo hivyo na majeruhi watatu.

Hii ni taarifa kamili.

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close