Android

Je, ni Salama Kusasisha “Update” Simu za Android Wakati Wote?

on

Mara nyingi tumekuwa tunakutana na swali hili kutoka kwa wasomaji wetu, wengi wanapenda kujua kama ni salama kuupdate simu za android kila mara simu zao zinapotaka wafanye hivyo.


Ili kupata huduma bora kutoka kwenye simu yako, ni wazo zuri kusasisha programu yako mara kwa mara. Toleo la hivi karibuni ya programu husaidia simu yako kufanya kazi kwa haraka zaidi na kwa ufanisi, inaleta vipengele vipya, kurekebisha bugs na zaidi.

Ndio, sasisho za hivi karibuni zinatolewa ili kurekebisha matatizo katika matoleo ya awali ya android, Mipangilio mipya hufanya kifaa chako kisiwe kwenye hatari zaidi ya kuvamiwa na wadukuzi pia huondoa virusi, bugs , glitches na vikwazo vya usalama ambavyo toleo la awali la Android linaweza kuwa navyo inaweka kifaa chako katika hali ya sasa ili uweze ku-install apps za hivi karibuni na kuhakikisha ufanyaji kazi bora wa apps mara nyingi toleo la karibuni la Android linafaa kwa apps na pia hujua na vipengele vipya na interface mpya.

SOMA NA HII:  Mfahamu Mwanzilishi Wa Kampuni ya Simu za Tecno - Tecno Mobile

Kuboresha programu yako ni mchakato wa bure na rahisi ambao hauchukua muda mrefu inategemea na njia iliyochaguliwa na kasi ya uunganisho wako.

 

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.