Nyingine

Sakata la Bosi wa UN kufukuzwa latua bungeni, Serikali yatoa ufafanuzi

Sakata la kufukuzwa nchini kwa bosi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Awa Dabo, limetua bungeni.

Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga (Chadema) akizungumza bungeni leo, aliitaka serikali kufafanua sababu za kumfukuza nchini Mkurugenzi Mkazi huyo wa UNDP Tanzania kwa kumpa saa 24.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge aliliambia bunge kuwa serikali ina mamlaka yote katika masuala ya kidiplomasia na hivyo bunge haliwezi kuhoji sababu za mkurugenzi huyo kufukuzwa.

Wakati huo huo, Serikali imefafanua kufukuzwa kwa bosi wa UNDP:-

Serikali imesema imefikia uamuzi wa kumuondoa nchini Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Awa Dabo kwa sababu mbalimbali ikiwamo ya kutokuwa na maelewano mazuri na watumishi wenzake.

Taarifa iliyotolewa leo na kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inasema maelewano hayo mabaya na watumishi wenzake yalizorotesha utendaji kazi wa shirika hilo.

SOMA NA HII:  80% watashindwa mchezo huu: ni Glass gani itajazwa kwanza?

Zinazohusiana

JIUNGE NA MAZUNGUMZO, TOA MAONI YAKO HAPA

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Lako