Habari za Teknolojia

Safaricom matatani nchini Kenya baada yakumbwa na matatizo ya mawasiliano

Kampuni kubwa ya mawasiliano nchini Kenya Safaricom imekumbwa na matatizo ya kiufundi ambayo yameathiri huduma zake za simu.

Safaricom imesema hitilafu hiyo imeathiri huduma zake kote nchini humo.

“Tunakabiliwa na tatizo la kuunganisha simu, data na huduma ya M-Pesa. Tatizo hili kwa sasa linaangaziwa. Samahani kwa usumbufu,” kampuni hiyo imeambiwa wateja kupitia Twitter.

Jina la kampuni hiyo limeanza kuvuma katika mitandao ya kijamii, wateja wakitaka kujua nini sababu yao kushindwa kupiga simu na kupokea au kutuma pesa.

Kampuni hiyo imeesema kiini cha matatizo hayo ni hitilafu katika hifadhi data yake ya GSM, teknolojia inayofanikisha mawasiliano ya simu za mkononi duniani.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya, asilimia 71.2 ya watu wanaotumia simu za mkononi Kenya hutumia mtandao wa Safaricom.

Kampuni hiyo ina jumla ya wateja 27.2 milioni wa simu za rununu.

Majibu ya Safaricom kwa wateja waliokuwa wakilalamikia kampuni hiyo kwenye Twitter
SOMA NA HII:  CIA imeonyesha "hard drives" za Osama bin Laden zenye video games, anime, na filamu za watoto

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.