Magari

Sababu za Magari ya Toyota Kuwa Maarufu Sana Tanzania

Hakuna asiyejua kwamba kampuni ya Toyota ina umaarufu kuliko kampuni zote za magari Tanzania, hata watoto wadogo ukiwaambia wataje magari wanayoyajua lazima utasikia neno “Toyota”. Kwa mujibu wa Best Selling Cars, 1 kati ya magari 4 yanayonunuliwa Tanzania ni Toyota.

Toyota

Wengi wamekuwa wakijiuliza mitaani, kwa nini Toyota ni maarufu sana Tanzania ? yani kila sehemu unayoenda ndani ya nchi hii utakutana na magari mengi ya Toyota kuliko kampuni zingine. Sasa, leo nimekusogezea sababu za kwa nini Toyota zinapendwa zaidi.

1. Gharama Nafuu

Toyota iliyotumika kidogo Japan ni gharama nafuu zaidi ya Ford au Jeep kutoka marekani au hata ukitaka kununua hapa hapa nchini. Pia, serikali ya Tanzania inawaruhusu wauzaji wenyeji kuingiza magari haya kwa gharama za chini zaidi. Kwa sababu, hata bei yake ya kununua ipo chini kulingana na magari mengine.

2. Hazitumii mafuta mengi

Magari ya Toyota yanajulikana kwa kutumia mafuta kidogo, nadhani magari madogo ya Toyota yanaongoza katika hili lakini hata magari yao makubwa mengine (Prado kwa mfano), hayatumii mafuta mengi ukilinganisha na magari makubwa ya makampuni mengine. Japo hili ni muhimu kwa watanzania wengi ambao maisha yao ni ya kawaida.

SOMA NA HII:  Kufikia 2040 China itakuwa imefikia hatua hii ya teknolojia ya magari

3. Upatikanaji wa spea

Kuna baadhi ya magari ukitafuta spea zake kama upo mikoani utaambiwa nenda dar es salaam na ukienda huko utaambiwa mpaka Mombasa. Hii ni tofauti kwa magari ya Toyota spea zake zipo kila sehemu nadhani kwa kuwa Toyota ni maarufu sana, spea zake zinapatikana kiurahisi zaidi pia, kitu ambacho kinapunguza gharama ya utunzaji.

4. Zina wataalam wengi

Karibu kila fundi wa magari ukimuuliza aina ya gari aliyojifunzia ufundi atakwambia Toyota, umaarufu wa Toyota umesababisha mafundi wengi wa magari kuwa na ujuzi wa magari ya Toyota.

Mtu mwenye gari la Hummer au Volkswagen Polo, kwa mfano, atapata shida sana kutafuta fundi mzuri na pia, matengenezo yatakuwa ya gharama kubwa zaidi.

5. Kuna aina ya gari kwa wote

Swala la kuchagua gari la kununua likijitokeza, watu wengi wanafikiria aina za Toyota na sio aina za magari. Toyota ina aina nyingi za magari zinazokidhi mahitaji ya watu mbalimbali. Kwa kifupi, mtu yoyote anaweza akaendesha Toyota.

Mchango wetu ni mkubwa kwenye umaarufu wa Toyota

Ukweli ni kwamba watanzania wanaamua kununua gari kutokana na mapendekezo ya familia au marafiki. Kwa kweli, kwa kuwa Toyota ni maarufu kuliko wengine ni rahisi sana kutafuta gari ya kampuni hiyo tu. Ila, kuna faida ya kuangalia magari ya makampuni mengine pia.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako