Sahau Linux: Sababu 10 Kwanini Unapaswa Kuendelea kutumia Windows


Umewahi kuwa na shida na Windows? Je, umewahi kuchanganyikiwa na njia “ya kipekee” ya Microsoft ya kusimamia faragha? Umewahi kujiuliza kwa nini Windows haitaki kuweka vizuri zaidi kifaa chako kipya ?

Unahitaji kutumia Linux badala yake. Ndio, ndivyo unavyoweza kuamini ikiwa unatumia muda mwingi kuvinjari mijadala ya mtandaoni (forums) au hata sehemu ya maoni kwenye tovuti).

Sahau Linux: Sababu 10 Kwanini Unapaswa Kuendelea kutumia Windows

Hata hivyo, hakuna kitu kinachoweza kuwa mbali na kweli. Ikiwa unafikiri juu ya kuhamia kwenye mfumo wa uendeshaji wa Linux, acha mpango huo sasa. Soma makala hii, kisha niambie kama bado ni uamuzi wa busara.

Hizi ni sababu 10 kwa nini ni bora zaidi kutotumia Linux. Ishi kwa muda mrefu Windows.

1. Ukosefu wa Programu

Unaangalia nini katika mfumo wa uendeshaji (operating system)? Kwa watu wengi, jibu labda ni urahisi wa matumizi na utangamano. Nitaangalia urahisi wa matumizi kwa ufupi. Kwa sasa, hebu tuzingatie utangamano.

Andika orodha ya programu unazotumia kila siku. Umemaliza ? Safi. Sasa linganisha na orodha hii ya programu ambazo kihalisia hazipatikani kwenye mifumo ya Linux (Linux systems):

  • Adobe Photoshop
  • Microsoft Office
  • Dreamweaver
  • 7-Zip
  • Final Cut Pro
  • Outlook
  • IrfanView

Ningeweza kuendelea, lakini siwezi. Nina hakika unapata wazo juu ya ninachokiongea. Watumiaji wa Linux hawawezi kutumia huduma ya baadhi ya programu nyingi sana zinazotumika kwa wingi. Ndiyo, katika hali fulani utaweza kupata njia au kutumia programu kama vile “Wine”, lakini mara nyingi haifanyi kazi katika ubora unaotakiwa na sio ya kuaminika. Ikiwa mtu anakuambia vinginevyo, ni uongo.

Ikiwa unathamini upande wa “kila kitu kinafanya kazi” kwenye Windows, usibadilishe.

2. Software Updates

Hata wakati programu ya Linux inapatikana, mara nyingi huwa nyuma ya mshirika wa Windows.

Kwa nini? Fikiria hili: Windows XP, 7, 8, na 10 kwa pamoja ni asilimia 85 ya kompyuta zote duniani leo hii. Na Linux? ni kiwango kidogo zaidi ya asilimia moja.

Chanzo cha picha: Wikipedia

Kwa hivyo, makampuni huwekeza rasilimali zao katika kuboresha Windows (na Mac) iliyotolewa kwanza kabisa. Hakika, kampuni kubwa sana zinaweza kujitolea fedha za R & D katika Linux kwa kiwango sawa kama Windows, lakini makampuni ya ukubwa wa kati (au watengenezaji binafsi) hawezi kufanya hivyo.

SOMA NA HII:  Fahamu Faida & Hasara za Kutumia Kompyuta ya Windows 8

3. Mgawanyiko

Ikiwa uko katika soko la mashine mpya ya Windows, una chaguo moja: Windows 10. Hakika, kuna tofauti kadhaa, kama vile Pro, S, na Enterprise, lakini zote kimsingi ni bidhaa sawa.

Lakini kama wewe ni mtumiaji wa mala ya kwanza na unatafuta mashine mpya ya Linux? Ni wakati wa kurudi shuleni. Kuna zaidi ya matoleo 250 tofauti ya Linux unayoweza kuchagua.

Unakiwa kujifunza matoleo kadhaa vizuri kabla ya kufanya chaguo sahihi. Kufanya mambo ngumu, baadhi yao ni usiku na mchana kwa suala la vipengele, interface ya mtumiaji, na urahisi wa matumizi.

Sibishani dhidi ya uchaguzi wa mtu moja kwa moja, lakini ukweli ni kwamba mgawanyiko wa Linux unachanganya sana, na hivyo hauwezekani, kwa watu wengi.

4. Bugs

Ndiyo, najua, Windows bado ipo mbali na kuwa kamilifu kabisa. Mfumo wa uendeshaji una “bugs”, na tangu Microsoft imebadilisha Windows 10 kuwa kitu kinachofanana na toleo la beta, masuala haya yamekuwa mabaya zaidi kuliko hapo awali.

Lakini angalia hivi: Windows 10 sasa inaendesha vifaa zaidi ya nusu bilioni. Watu wengi hawana matatizo yoyote.

Kwa nini isiwe hivyo? Kwa sababu Microsoft ina bajeti na huajiri mamia ya watu ambao kazi yao pekee ni kupima na kusafisha mfumo wa uendeshaji (operating system). Linux haifanyi hivyo. Hata “distros” zinazotumika kwa kiasi kikubwa kimsingi huendeshwa na kundi la wapendaji kazi hiyo katika bajeti ndogo.

Kwa watu wenye ujuzi, “bugs” inaweza kuwa si tatizo; wana ujuzi wa kutosha kutambua na kutatua matatizo wenyewe. Kwa watumiaji wa kawaida, kutatua matatizo ya Linux (troubleshoot Linux) itakuwa shida.

Ikiwa umefanya asilimia 85 ya dunia kuanza kutumia kompyuta yenye mfumo wa Linux , nakuhakikishia kuwa utaona maada nyingi watu wakilalamika kuhusu mambo ambayo hayafanyi kazi sawasawa kuliko unavyoona kwenye Windows.

5. Msaada

Ikiwa kitu fulani kinaenda kinyume kabisa na mashine yako ya Windows, una fursa kadhaa zilizofunguliwa kwajili yako. Microsoft yenyewe hutoa mazungumzo ya maandishi(text chat) na msaada wa simu, wakati kila mfanyakazi wa duka la kutengeneza PC nchini hufahamu vyema mfumo huu wa uendeshaji na jinsi unavyofanya kazi.

Ikiwa unatumia Linux, umejifunga kwa makampuni kadhaa ya wataalam na majadiliano ya mtandao (forums) ya kujitolea. Na ikiwa hujui, “forums” sio maeneo rahisi ya kupata msaada ikiwa wewe ni mtumiaji wa kawaida “noob”.

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kuondoa "This copy of windows is not genuine" Kwenye Kompyuta Yako

6. Drivers

Windows kawaida hupata “drivers” mapya kwanza, ikifuatwa kwa karibu na macOS. Mfumo wa Linux una bahati ikiwa unapokea “drivers” yoyote. Ila jumuiya ya Linux inaendelea drivers za chanzo cha wazi (open-source drivers) ambazo husafiri na Linux distros.

Mimi sipingani na watu wanaofanya kazi ya kutengeneza “drivers” kama hizo; kwa kiasi kikubwa wanafanya kazi kubwa. Lakini ukweli ni mara nyingi zinakuwa hazijakamilika au hazina baadhi ya sifa. Na kwa sababu hawana usaidizi rasmi wa kampuni mama, hawatapokea msaada wowote ikiwa hawawezi kufanya kitu fulani kifanye kazi.

Tena, kwa “fanatics wa Linux”, sio tatizo – ni sehemu ya furaha. Lakini kwa watumiaji wa kawaida wa nyumbani wanaotaka tu kompyuta ifanye kazi, hali hiyo itawasumbua sana.

7. Games (Michezo)

Huenda hii ni hoja inayozungumzwa mara nyingi katika mijadala ya Linux, na kwa sababu nzuri. Michezo mingi haifanyi kazi kwenye Linux na kwa sababu hiyo haifai kuwekeza muda kwenye utengenezaji.

Hali hiyo inabadilika. Steam imekuwa ikifanya kazi kwa bidii ili kuweka michezo kwenye Linux, lakini bado ni njia ndefu kuwa sawa na Windows.

8. Peripherals

Hii ina uhusiano wa karibu na masuala yanayozunguka michezo ya kubahatisha (gaming). Hata kama unaweza kupata michezo yako unayoipenda, kuna uwezekano mkubwa huwezi kudhibiti vitendo kwenye skrini kwa kutumia vipengele vyako vilivyopo. Katika hali nzuri zaidi, msanidi programu wa Linux (Linux developer) atakuwa na usaidizi wa kuingiliana kwao.

Tatizo la “peripherals” pia huongeza njia zaidi ya michezo ya kubahatisha. Hata kitu muhimu kama kadi yako ya Wi-Fi inaweza kukupa shida wakati unapoweka toleo la linux kwa mala ya kwanza. Je, unataka kutumia masaa kukabiliana na “commands”, repos, na vyanzo mbalimbali, ili uweze kuingia mtandaoni? Tena, kwa watu wengi, jibu ni hapana.

9. Ugumu

Linux ni ngumu. Usiseme sio. Ni ngumu! Na sio tu nazungumza juu ya mpangilio wa desktop au wapi unaweza kupata mipangilio (settings) mbalimbali – mtumiaji mpya anaweza kuelewa kwa kasi mambo hayo kwa siku chache.

SOMA NA HII:  Format memory card, flash drive (Njia ya kuondoa virus kabisa)

Ninazungumzia kuhusu kutumia mfumo wa uendeshaji (operating system) wa kila siku. Ikiwa umetumia Linux kwa miaka 20, basi hakika inaonekana rahisi. Kwa mtu anayekuja kutoka kwenye programu ya Windows, hata kitu rahisi kama kuweka (install) programu inahitaji utafiti. Sio sahihi.

Mfumo wa uendeshaji wa Linux wa kweli haujawahi kumalizika, mambo daima huvunjika na kuwepo haja ya kuyarekebisha. Watumiaji wengi wa kawaida hawana muda au uelewa wa kompyuta zao.

Wakati kundi kubwa la teknolojia linapochagua Linux na kuendesha mfumo wao – kama Google na Chrome OS yake – matokeo yanaweza kuwa ya ajabu. Lakini matoleo mengine unayotaka kuyatumia hayafikii hatua hiyo ya urahisi wa matumizi.

10. Kuinstall Linux Ni Ngumu

Tena, ikiwa unasoma hii na kutikisa kichwa chako, wewe ni sehemu ya watu wachache. Usifikiri kila mtu ana ujuzi wa teknolojia kama wewe. Kwa watumiaji wengi, wazo la kuunda “bootable USB drives” au “installation CDs” ni mtihani mkubwa.

“Dual booting ” (ambayo, ikiwa ni mtumiaji wa Linux kwa mara ya kwanza na ana kompyuta moja tu, ni vigumu zaidi kuelewa.

Bila shaka, Ubuntu ni moja ya programu mpya zinazopatikana kwenye Windows Store, hivyo jambo hilo linasaidia kufanya Linux kupatikana zaidi. Lakini ikiwa hutumii Windows 10, au unataka kukimbia “distro” zisizo za Ubuntu, ni vigumu kuliko unavyofikiria.

Linux (labda) Sio kwa ajili yako

Sikia, sio kwamba Linux ni mbaya kabisa. Ikiwa wewe ni mtu mwenye uelewa wa teknolojia ambaye anapenda kutumia maujanja, huenda utafurahia sana kuitumia. Ina salama zaidi kuliko Windows na kwa njia nyingi, ni “customizable” zaidi.

Hata hivyo, kama wewe ni aina ya mtumiaji ambaye anapenda kubonyeza kitufe cha kuwasha kompyuta tu na kuona kila kitu kinafanya kazi vizuri na bila vikwazo, unapaswa kutoitumia. Ikiwa unadhani Windows mara kwa mara inakupa maumivu ya kichwa, hujaona kitu chochote bado.

Umejaribu Linux? Je, umeshikamana nayo au umerudi kwenye faraja ya mazingira ya Microsoft? Kwa nini unadhani watumiaji wengi wa Windows watakuwa wapumbavu kufanya mabadiliko? Unaweza kuacha mawazo na maoni yako yote katika sehemu ya maoni hapa chini.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA