Sambaza:

Rais wa Urusi Vladimir Putin amepitisha sheria mpya ambayo itapiga marufuku mitandao ya kibinafsi na teknolojia nyingine ambazo hutoa upatikanaji usiojulikana wa wavuti, TechCrunch imeripoti.

Kitengo cha habari cha serikali ya Urusi-RIA kimeripoti kuwa mwenyekiti wa kamati ya sera na teknolojia ya habari, Leonid Levin, amesema sheria haikusudia kuanzisha vizuizi vipya kwa wananchi kuhusu utumiaji wa mtandao. Itaanza kutumika tarehe 1 Novemba.

Serikali ilipitisha sheria mwaka 2015 ambayo inahitaji data zote za watumiaji wa mtandao nchini Urusi zihifadhiwe ndani ya nchi hiyo. Mnamo mwaka wa 2016, ilipitisha sheria ambayo inasababisha watoa huduma za mawasiliano na watoa huduma za mtandao kuhifadhi habari za trafiki mtandao (network traffic information) hadi mwaka mmoja.

Hii imesababisha watoa huduma za VPN Private Internet Access kufunga huduma zao nchini Urusi.

Habari za kupiga marufuku zimefuatia taarifa kwamba Apple imefuta apps kubwa za VPN kwenye App Store nchini China. Hii ilifanyika ili kuzingatia kanuni ambazo zinasema kuwa programu zinapaswa kuidhinishwa na serikali ya Kichina.


Sambaza:
SOMA NA HII:  Top 10 ya Movies Zilizopakuliwa Zaidi Kupitia Torrent Wiki Hii

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako