Nyingine

Ruksa Media Kuikosoa Serikali, Je Tanzania Tuna “Strong Media” au “Strong Journalists” wenye Uwezo huo?

Serikali ya Tanzania imetoa ruhusa kwa media kuikosoa Serikali ila ili hili liweze kufanyika kwa manufaa na kuleta tija, lazima kwanza tuwe na Independent Strong Media na tuwe na waandishi mahiri ambao ni “Iconic figures akiandika “This is wrong”, Serikali itasikiliza”.

Swali ni je Tanzania tunazo hizo “strong media” ?, je tunao hao “strong journalists” wenye uwezo wa kuikosoa Serikali na Serikali ikawasikiliza?.

Kama tunazo ni zipi? . Kama hatuna kwa nini hatuna strong media?. Na je hao strong journalists tunao ?, ni kina nani wakiandika au wakisema Serikali itasikia, itabadilika?.

Mifano ya Strong Media.
Marekani wana strong media, wana vyama viwili vikuu vya siasa Democrats na Republican, wana magazeti makuu mawili, The New York Times na The Washington Post pia wana TV mbili kubwa CBS na ABC.

Uingereza pia wana Strong Media, wana vyama vikuu viwili vya siasa Labour na Conservative, wana gazeti moja kuu, The Daily Telegraph pia wana radio moja kuu na TV moja kuu, BBC.

Sisi tuna utitiri wa vyama, utitiri wa magazeti na utitiri wa TV stations, je tuna any strong media ndani ya utitiri huu?…

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close