Rudisha Vitu/Data zako Zilizopotea Katika Flash/External HDD Kwa Urahisi


Je ulishawahi kukutana na tatizo la kupotea kwa data zako kwenye flash au External hard disk?ternal hard disk yako kwenye Kompyuta inaonyesha ina  vitu/data ila ukifungua haukuti kitu?

UFAFANUZI;

  • Kwanza hupaswi kuformat flash/external hard disk yako
  • Kwa sababu vitu vyako vipo salama kabisa
  • Vitu vyako vimefichwaa na aina yaVirus anayeitwa “Skypee” (aina ya virusi inayounda njia za mkato za faili na folda na ina uwezo wa kuficha faili za awali)

Kufanya Vitu Vyako Vionekane Na Kutumika Tena Bila Tatizo Lolote Fuata  Hatua Hizi:

1. Kwanza hakikisha una programu/USB antivirus iitwayo SMADAV (kama hauna basi download kwa kutumia link hii hapa pakua Smadav bure)
2. Install katika Kompyuta yako.
3. Chomeka/insert flash au external hard disk kwenye kompyuta ambayo ina Smadav.
4. Right click katika flash/hard disk halafu bonyeza “scan with Smadav”

Rudisha Vitu/Data zako Zilizopotea Katika Flash/External HDD Kwa Urahisi5. Ikianza kuscan tu utaona hapo kulia chini kwenye desktop kuna notification yake imetokea, maximize/ikuze ionekane kwa upana, ili uweze kuona inavyoscan.
6. Baada ya kumaliza kuscan kuna sehemu utaona imeandikwa “fix all” basi click hiyo sehemu.


7. Subiri kidogo, ikimaliza kuondoa hao wadudu ifunge.
8. Sasa ukifungua flash utaona “folder” ambalo halijaandikwa jina, lifungue, utakuta vitu vyako vyote, “cut, na kisha paste” nje ya folder hilo kisha futa folder hilo lisilo na jina.Vitu vyako vipo salama kabisa.

Ningependa kusikia kutoka kwako, Umejaribu kutumia njia hii ? Vile vile niandikie hapo chini sehemu ya comment ni njia gani wewe unatumia kurudisha data zako zilizopotea?

Kwa Habari Zaidi Na Maujanja Mbalimbali Ya Teknolojia Endelea Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa Mediahuru Kila Siku Kwani Daima Tunaaminika Katika Teknolojia!

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA