Nyingine

Breaking News: Roma apatikana, yupo kituo cha polisi Oysterbay

on

Taarifa zilizotufikia zimedai kuwa Roma na watu wengine waliokuwa wameshikiliwa tangu Jumatano hii wamepatikana wakiwa salama.

Habari ya Roma na wenzake  kupatikana imethibitishwa na Mkurugenzi wa Tongwe Records J. Mada

Bado hakuna maelezo ya kutosha kuhusiana na wapi walipokuwa na nani waliokuwa wamewashikilia. Kwa sasa wanaidaiwa kuwa katika kituo cha polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa taratibu za kipolisi kwakuwa jalada la kupotea kwao lilifunguliwa hapo.

Kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na mashabiki kuhusu kuachiliwa huru, ndani na nje ya mitandao ya kijamii.

Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake.

About Benix Matrix

Leave a Reply

Your email address will not be published.