Biashara MtandaoniHuduma za Mtandaoni

Ringier imenunua hisa 100% za BuyrentKenya, Sasa kushindana Afrika Mashariki

BuyRentKenya sasa imenunuliwa na Ringier One Africa Media na itaingia katika ROAM (ushirikiano unaotaka kufanyika  kati ya Ringier na One Africa Media) katika hatua ya kujenga kundi kubwa barani Afrika la classifieds.

Jamie Pujara, Co-founder na Mkurugenzi Mtendaji wa BuyRentKenya amesema yeye na mshiriki wake wataiacha kampuni hiyo na kuwekeza muda wao katika changamoto mpya na Lizzie Costabir (ambaye ndiye meneja wa sasa wa masoko atasimamia kampuni hiyo chini ya ROAM.

“Mimi na Nico tunafurahi sana kwamba BuyRentKenya itaunganishwa kikamilifu katika ROAM. Tunaimani na uongozi wao, utaalamu na uzoefu wao utafikia hatua kubwa katika kutambua maono yetu ya kufanya utafutaji wa mali na kuorodhesha bidhaa kuwa rahisi na uwazi zaidi nchini Kenya, ” Jamie aliiambia TechMoran.

Ilianzishwa mwaka 2012, na Jamie Pujara na Nicolas Adamjee, Malengo ya BuyRentKenya.com yalikuwa utafutaji wa mali na orodha ya bidhaa mbalimbali kuwa rahisi zaidi, wa kuaminika na yenye uwazi zaidi. Mnamo Machi 2014, kampuni hiyo ilipokea kiasi cha fedha ambacho hakijulikani kutoka kwa One Media Media kwa ajili ya hisa ndogo baada ya mfululizo wa wasimamizi kushindwa kuendana  na mahitaji ya wamiliki.

Katika kipindi cha miaka 5 tangu wawili hao waanzishe kampuni, tovuti hiyo imekuwa na watembeleji zaidi ya milioni 5, imeingia kwenye ushirikiano na mashirika zaidi ya 500, imeorodhesha zaidi ya mali 50,000 mtandaoni na kukuza uwekezaji kutoka kwa One Africa Media (OAM) ambao ni muhimu sana.

SOMA NA HII:  Hatua za Usalama Wakati Wa Kufanya Ununuzi Mtandaoni "Online"

ROAM hivi karibuni ilinunua mali za Media One Afrika nchini Kenya, Nigeria na sehemu nyingine kadhaa za Afrika kama vile Cheki lakini One Africa Media ilikuwa na hisa chache katika BuyRentKenya na PrivateProperty ya Afrika Kusini. Kampuni hizo mbili zinazojihusisha na biashara ya mtandaoni hawakukubaliana na hesabu ya awali ya ROAM kuhusu thamani ya mali zao na walifanya kazi kwa kujitegemea ndani ya chombo kipya. PrivateProperty ilipata mnunuzi kutoka Naspers. Huku BuyRentKenya ikichukuliwa na ROAM na hii ni habari njema kwa timu zote pamoja na ROAM. BuyRentKenya ilihitaji mshirika ili kushindana kwa ufanisi na Jumia House zamani iliitwa Lamudi na wawekezaji wengi wapya wanatazama soko la Afrika Mashariki baada ya PropertyLeo kufa.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako