Home Nyingine Rich Mavoko Asajiliwa Rasmi na label ya Diamond

Rich Mavoko Asajiliwa Rasmi na label ya Diamond

0
0

Mwanzo zilikuwepo tetesi kuwa Msanii Rich Mavoko ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake ‘Naimani’ kuwa amesaini mkataba wa kusimamiwa kazi zake chini ya Label ya WCB ambayo ipo chini ya msanii Diamond Platnum.

Tetesi hizi ziliendelea kubaki tetesi hadi jana ambapo imewekwa wazi kuwa ni kweli msanii huyo hivi sasa yupo chini ya WBC.

Kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio msanii Harmonize alithibitisha kuwa ni kweli Rich Mavoko kwa sasa yupo chini ya label hiyo ambayo mpaka sasa ina wasanii kadhaa akiwepo yeye mwenyewe Harmonize, Raymond aliyekuwa Tip Top Connection pamoja na Rich Mavoko.

“Unajua mwanzo zilikuwa ni tetesi lakini naweza kusema ‘its official’ sasa Rich Mavoko yupo chini ya WCB, hivyo kusema kuwa Rich Mavoko amenyoosha mikono kwa Diamond si vizuri kwani watu wanaweza kupata picha tofauti maana si unajua watu wanaweza kupokea jambo kwa maana na ikaleta picha mbaya wakati ni jambo la kawaida” alisema Harmonize

Lakini mbali na hilo msanii huyo amedai kuwa mwezi wa tatu anatarajia kuachia albam yake ya kwanza na kusema ameamua kuachia albam hiyo kwa lengo la kujitengenezea CV katika muziki.

“Tumekaa na uongozi wangu mwezi wa tatu nitaachia albam yangu ya kwanza hivyo kwenye label yangu nitakuwa msanii wa kwanza kutoa albam lakini nafanya hivi ili kupata heshima maana bila kuwa na albam huwezi kumwambia msanii mkubwa wewe ni msanii mkubwa Afrika Mashariki wakati huna albam hata moja, hivyo natoa albam yangu nipate heshima na si kwa ajili ya mapato” alisema Harmonize

(0)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *