Nyingine

RC Makonda aagiza nyumba 36 kubomolewa bonde la mto Msimbazi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam leo amefanya ziara kwa wakazi wanaoishi kwenye bonde la mto Msimbazi ili kujionea athari mbalimbali zilizotokea kwenye mafuriko.

Makonda amezitembelea nyumba hizo katika Kata ya Bugurni kwa Mnyamani na Tabata , akiwa na vikosi vya ulinzi na usalama ambapo ameshuhudia maafa makubwa yakiwemo ya baadhi ya watu kupoteza mali pamoja na nyumba zao kujaa maji.

Mkuu wa mkoa amewashukia wakazi wanaoishi bonde hilo waliojenga nyumba na kuziba mto, ukuta ulioziba mto na kuamuru halmashauri kubomoa nyumba hizo 36 bila kulipa fidia kuanzia kesho.

RC Makonda amesema kuna watu ambao tayari wamelipwa pesa kuhama maeneo hayo lakini cha ajabu wengine hawajaondoka na wengine wamewapangisha watu wengine kwenye maeneo hayo hatarishi, jambo ambalo serikali yake haiwezi kulikalia macho na kuagiza kubomolewa kwa nyumba hizo.

Pia amewataka wale ambao hawajahakiki taarifa zao kuhusu kupewa hifadhi baada ya nyumba zao kubomolewa wafanye hivyo kwa kwendaq ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa uhakiki huo.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close