Sambaza:

Unataka kujua simu ya kuchezea magemu inakuwa na muonekano gani ?

Naam, jibu ni hili hapa:

Razer, kampuni inayojulikana kwa kutengeneza magemu, imeingia kwenye utengenezaji wa simu janja na matokeo yanaonekana kuwa mazuri (ukiangalia sifa zake kiundani). Hivi ni baadhi ya vitu vinavyopatikana kwenye simu hiyo:

  • Prosesa: Qualcomm Snapdragon 835
  • Diski Ujazo: 64GB, Unaweza kuweka mpaka memori ya ukubwa wa 2TB
  • RAM: RAM ya 8GB
  • Kioo: 5.7-Inch IGZO LCD, 1440×2560
  • Kamera ya nyuma (Rear): 12-megapixel
  • Kamera ya mbele (Selfie): 8-megapixel
  • Betri: 4,000 milliamp
  • Ukubwa: 158.5 x 77.7 x 8 mm/6.24 x 3.06 x 0.31-inches
  • Programu Endeshi: Android Nougat 7.1.1
SOMA NA HII:  Njia 5 za Kufanya Kuchat Kuwe na Mvuto Zaidi

Simu janja kutoka Razer imejidhatiti hasa kwenye RAM, ina RAM GB 8 (kuepuka kukwamakwama unapokuwa unacheza gemu) ambayo ni RAM ya kiwango cha juu sana kulinganisha na simu janja nyingi zilizotoka hivi karibuni ambazo zenye kiwango cha juu kabisa ni GB 6.

Kampuni hiyo pia imejumuisha mfumo wa sauti unaofanya kazi na Dolby Atmos. Kama hiyo haitosha, Razer wameongeza 24-bit DAC, ambayo haina maana kwamba kuna sehemu ya kuweka  “headphone” , kwa sababu hakuna sehemu hiyo kwenye simu ya Razer. Kitufe cha kuwashia simu kwenye simu ya Razer pia kinaweza kutumika kama fingerprint sensor.

Ingawa kampuni inadai kwamba imefanya hivyo kwa sababu inatarajia watumiaji kutumia simu hiyo katika “landscape mode” muda mwingi.

Kwa sasa, simu ya Razer inapatikana katika rangi moja (Nyeusi) na inatarajiwa kuuzwa  kwa $ 699 (Karibu Tsh 1,569,000).

Ndiyo, simu inaonekana kama kitu kutoka mwaka 2016, lakini je, sifa na bei ni nzuri kwako?


Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako