Sambaza:

Rais Magufuli :

 • TCRA wanatoa faini ndogo na inawafanya makapuni ya simu yaendelee na ukwepaji kodi. Mimi nawaambia TCRA makampuni yasiyotaka kulipa kodi, Futa kabisa hiyo kampuni.
 • Ni lazima kila mmoja alipe kodi; awe anataka au hataki. Niwaombe makampuni muingie katika hii data centre. Kama mtu unalipa kodi unaogopa nini kujiunga na mfumo huu?
 • Wale walio chini yangu wala siwaombi na naomba makamu wa Rais ukasimamie hili.
 • Mtu anaponunua vocha au kufanya transaction ya pesa ameshalipa kodi, Peleka hiyo VAT kwa serikali.
 • Ethiopia ina kampuni moja ya simu ila sisi Tanzania tuna kampuni zaidi ya saba za simu.
 • Nitolee mfano mdogo tuu, Tanzania tungekuwa na senta moja ya kupima na ku-lebel dhahabu tungepata mapato mengi sana.
 • Tungeanzisha hata vitambulisho vya machinga na tukaviuza kwa shilingi elfu kumi tungepata mapato mengi sana.
 • Kodi za nyumba watu hawalipi kwasababu hamna utaratibu mzuri
 • Hata hivyo nawapongeza sana vijana waliobuni mfumo huu, japo mmesema wanamefanya bure lakini najua wanalipwa mshahara. Jinsi mfumo huu utavyoendelea kusaidia kukusanya mapato tutawafikiria kuwaongeza mishahara.
 • Najua tuna data centre nyingi. Sasa nisione wizara au idara ikijenga data centre nyingine
 • Niwaombe makampuni, wafanyabiashara mjiunge na mfumo huu.
 • Naomba nimshukuru sana Rais wa Zanzibar Dr Shein, Makamu wa rais, waziri wa fedha, waziri wa mawasiliano
 • Narudia wito wangu kwa kuwaomba sana sana, ndugu zangu wenye makampuni ya simu muwe wa kwanza kujiunga na mfumo huu. Mimi mwenyewe namiliki laini ya Vodacom, Airtel, Tigo na TTCL.
SOMA NA HII:  Vanessa Mdee amezindua ‘app’ ya simu ya Vee Money

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako