Nyingine

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha kupisha uchunguzi

RAIS John Magufuli ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Shirika Elimu Kibaha Dkt. Crispin Mpemba ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali za kiutendaji zinazomkabili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Simbachawene amesema kufuatia tuhuma mbalimbali za uendeshaji, zinazolikabili Shirika hilo ambazo zimekuwa zikiandikwa kwenye vyombo vya habari kwa muda mrefu sasa.

Simbachawene amesema Mnamo Machi, 4 mwaka huu Rais Magufuli ametengua rasmi nafasi ya Mtendaji huyo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo.

Amefafanua kuwa kumekuwepo malalamiko dhidi ya Mtendaji Mkuu wa wa shirika la Elimu Kibaha ambapo Ofisi ya Rais TAMISEMI iliunda kikosi kazi ili kufanya uchunguzi dhidi ya malalamiko hayo na kugundua kuwepo kwa changamoto katika uendeshaji wa Shirika hilo.

“Ni kweli tuhuma juu ya uendeshaji wa Shirika la Elimu Kibaha likiwemo suala la Mikataba iliyoingiwa na Shirika hilo zimekuwepo kwa muda mrefu sasa. Sisi kama Wizara hatukutaka kukurupuka kufanya maamuzi na tukaamua kuunda kikosi kazi ili kufanya uchunguzi na matokeo ya uchunguzi huo yanapelekea kuwepo kwa hoja zinazohitaji uchunguzi zaidi,” ameeleza Waziri Simbachawene

Ameongeza kuwa ili uchunguzi huo uweze kufanyika kwa uhuru Mhe. Rais ameamua kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha ili kupisha uchunguzi wa kina dhidi yake.

Waziri amesema uamuzi wa kumsimamisha umechukuliwa kwa kuwa tuhuma na malalamiko mengi ya awali yaliyojitokeza dhidi yake yanajenga hoja ya kuhitajika kufanyika kwa uchunguzi zaidi ambapo kwa sasa nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha inakaimiwa hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *