Nyingine

Rais Magufuli amempigia simu Mwana FA, anaupenda wimbo wa ‘Dume Suruali’

Staa wa muziki wa hip hop bongo “Mwana FA”, jana jioni alitoa taarifa kupitia ukurasa wake wa twitter kuonyesha kufurahisha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kumpigia simu.

Rais Dkt John Magufuli ni shabiki wa muziki wa Mwana FA. Na ndio maana ameamua kumpigia simu rapper huyo kumwambia kuwa ni msikilizaji mzuri wa ngoma zake na amemweleza kuwa wimbo anaoupenda ni Dume Suruali aliomshirikisha Vanessa Mdee.

“Nimefurahi kupokea simu ya Mheshimiwa Rais @MagufuliJP kunisalimia na kuniambia yeye ni mpenzi wa kazi zangu,haswa #DumeSuruali,” ametweet Mwana FA.

“Utoe heRa kwani ina tv ndani?” (in his voice) 😀😂…,” ameongeza FA.

SOMA NA HII:  80% watashindwa mchezo huu: ni Glass gani itajazwa kwanza?

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.