Nyingine

Rais Donald Trump amemfuta kazi mkurugenzi wa shirika la ujasusi la FBI

Rais Trump na james Comey wa shirika la FBI wakisalimiana katika mkutano wa awali

Rais Donald Trump amemfuta kazi mkurugenzi wa shirika la ujasusi la FBI kutokana na hatua yake ya kuliangazia swala la barua pepe za aliyekuwa mgombea wa uraisi wa chama cha Democrat Hillary Clinton, mamlaka imesema.

Lakini wanachama wa Democrats wamesema kuwa alifutwa kazi kwa sababu FBI ilikuwa ikuchunguza madai ya uhusiano kati ya Trump na Urusi.

Hatua hiyo inajiri baada ya kubainika kwamba bwana Comey alitoa habari za uongo kuhusu barua pepe za Clinton kwa bunge la Congress wiki iliopita.

Rais Trump aliandika barua kwa bwana Comey kwamba alikubaliana na mapendekezo ya mwanasheria mkuu Jeff Sessions kwamba ameshindwa kuliongoza vizuri shirika hilo.

Naye kiongozi wa chama cha Democratic katika Bunge la Seneti, Bwana Chuck Schumer, amesema kuwa ni wakati mwafaka sasa kumteua kiongozi maalumu wa mashtaka kusimamia uchunguzi huo juu ya uhusiano na Urusi.

Alisema kuwa hatua hiyo isipochukuliwa raia wa Marekani wana haki ya kuwaza kuwa Bwana Comey amefutwa ili kupunja juhudi za kukamilisha uchunguzi huo.

Ikulu ya White House imekanusha kuwa kutimuliwa kazini kwa Bwana Comey kuna uhusiano wowote na maswala ya kisiasa.

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close