Sambaza:

Hatimaye Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imetoa kibali kwa radio pendwa hivi sasa kwa Dar Es Salaam 93.7 Efm kuanza kurusha matangazo yake kwenye mikoa Tisa ya Tanzania Bara.

Akiongea mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa niaba ya mkurugenzi wa EFM na TVE, General Manager wa EFM, Dennis Ssebo amesema TCRA imeipa kipali kituo hicho kuanza kurusha matangazo yake kwenye mikoa tisa ya Tanzania.

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imeipa kibali EFM kwenda mikoani na tunaingia kwenye mikoa tisa. Hiyo ndio habari kubwa ambayo mkurugenzi wa EFM alitaka kuzungumza na wananchi hii leo ni kwamba tumepewa ridhaa ya kwenda kwenye mikoa tisa. Mikoa hiyo ni ifuatayo Mbeya, Tanga, Mwanza, Mtwara, Manyara, Singida, Kigoma Tabora na Kilimanjaro.

Naye waziri Nape Akitoa hotuba yake amesema kuwa hakuwa anategemea kuona uwekezaji mkubwa uliofanywa na kituo hicho ambao ameuona na kutoa pongezi nyingi kwa bosi wa kituo hicho DJ Majay.

Mnavyoonekana nje sivyo mlivyo ndani. Ndani kuna uwekezaji mkubwa wa teknolojia kubwa na hakika gharama iliyotumika kuwekeza hapa ni kubwa sana, sisi kama serikali tunakupongeza sana na tunakutakia kila la kheri. Na ninakuahidi serikali tutakupa ushirikiano na msaada unaouhitaji kuhakikisha uwekezaji huu unasonga mbele, amesema Nape

Hakika sasa hapa kutakua na ushindani wa dhahiri kwa radio stations nyingine ambazo zilikua zimejiimarisha mikoani kama RFA,Radio One,Clouds fm,East Africa radio,Capital Radio na TBC fm.

SOMA NA HII:  Je una bashiri "kubeti" ili kujikwamua na matatizo ya kimaisha ?


Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

This article has 1 comment

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako