Programu ya Kuchati ya AIM Kufungwa Baada ya Miaka 20


AOL Instant Messenger ni programu tumishi ambayo imekuwa ikitoa huduma ya watu kuwasiliana kwa ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kwa njia ya intaneti kwa takribani miaka 20 sasa.

Programu ya ujumbe kwa njia ya mtandaoni, ambayo mara nyingi hujulikana kama AIM, itaondolewa/itafungwa rasmi desemba 15, kwa mujibu wa Michael Albers, Makamu wa Rais wa bidhaa za mawasiliano wa Oath, ambaye siku ya Ijumaa alitangaza mpango wa kuifunga programu hiyo.

Programu ya Kuchati ya AIM Kufungwa Baada ya Miaka 20
Taarifa rasmi kutokwa kwa AOL kuhusu kufungwa kwa programu ya AIM

AIM awali ilianzishwa kama sehemu ya programu ya mazungumzo iliyopo kwenye AOL desktop. Ilizinduliwa kama programu inayojitegemea mwaka wa 1997, na ikaendelea kuwa kubwa hata wakati ambao washindani kama Yahoo Messenger na MSN Messenger walipokuja. Lakini hadi mwaka wa 2011, mazungumzo ya Facebook na Google ya barua pepe, inayojulikana kama Google Chat au “Gchat” kwa kifupi, yalivutia watumiaji kwa kiwango kikubwa.

Ingawa programu hiyo itaacha kufanya kazi katikati ya mwezi Desemba ila huduma ya barua pepe iliyo chini ya AIM (mfano@aim.com) itaendelea kufanya kazi kwa sababu huduma ya kutuma na kupokea ujumbe wa maandishi tu ndio itafungwa.

Tuambie, wewe umeshawahi kutumia programu ya AIM? Je, habari hii ya kufungwa kwake umeipokeaje ?

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *