Je Kuna Programu ya Windows Unatamani Kuitumia Kwenye Simu ya Adroid ?


Mapema wiki hii, iliripotiwa kuwa toleo la hivi karibuni la Wine, programu ambayo inafanya iwezekane kutumia programu za Windows kwenye vifaa vya Apple na kompyuta za Linux itaanza kupatikana kwenye Android, hii ina maana kwamba utakuwa na uwezo wa kutumia programu za Windows 7 kwenye vifaa vyako vya Android.

Baadhi ya techies mtandaoni wameshangaa sana:

Sababu ni kwamba tuna programu nyingi za Android ambazo zinaweza kutumika kama mbadala wa programu maarufu za Windows, pia programu nyingi kwenye Windows store ziko pia kwenye Google Play.

Hata hivyo, bado nimefurahi kuhusu matarajio ya ku-install programu moja kwenye simu yangu, ambayo ninaitumia kwa ajili ya uhariri wa sauti—Audacity, programu ya kompyuta kwajili ya kurekodi sauti ambayo inapatikana kwenye Windows na MacOS tu .

SOMA NA HII:  Facebook kufanya utafiti ili kuboresha habari zake

Mbali na hiyo, hakuna programu ya Windows tu inayokuja kwenye akili yangu, vipi kwa upande wako, kuna programu ya Windows unatamani kuiweka kwenye kifaa chako cha Android ?

P.S. Unaweza kushusha Wine 3.0 kwa kutumia kiungo hiki (sio salama sana).

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA