Nyingine

Premier League !! West Ham vs Chelsea Siku ya Jumatatu (Toa Utabiri wako !!!)

Jumatatu usiku kutakuwa na London Derby itakayowakutanisha West Ham na Chelsea katika uwanja mpya maarufu wa London Stadium, Huku Chelsea ikitaka kuongeza point kuelekea ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza.

West Ham nayo inaonekana imefanikiwa kutoroka kwenye mbio za kushuka daraja, miezi ya karibuni wamekuwa wakicheza kwa morali kubwa na kupata matokeo mazuri licha ya kuondoka kwa Dimitri Payet.

Chelsea, kwa upande mwingine, wamekuwa wakifanya vizuri sana msimu huu, wanaelekea mechi ya tisa mfululizo bila ya kufungwa tangu kupoteza record yao ya michezo 13 baada ya kufungwa na Tottenham mwezi Januari.

West Ham wanaweza kujipa matumaini ya kushinda kwa kuwa walikifunga kikosi cha Antonio Conte 2-1 kwenye EFL Cup msimu huu, ushindi wao mkubwa mapaka sasa kwenye uwanja wao mpya.

Kuhusu Team-

Chelsea kwa mara nyingine tena itaingia uwanjani ikiwa na kikosi imara, ubora wa kikosi chake unaongeza chachu za kujiimarisha kileleni mwa ligi.  Wakati Diafra Sakho amerejea mazoezini, na Andy Carroll – ambaye ana rekodi nzuri dhidi ya Blues atakuwepo pia. Bado hakuna taarifa kamili kama beki wa zamani wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa atakuwepo kwajili ya mchezo huo.

Angelo Ogbonna, Gokhan Tore na Doneil Henry wataendelea kuwa nje msimu mzima, huku Michail Antonio akiwa suspended baada ya kuapata kadi ya pili ya njano kwenye mchezo dhidi ya Watford wikendi iliyopita.

West Ham haionyeshi dalili za kuisumbua chelsea  kwa sababu wachezaji wake wengi wanaonekana wako nje ya form, lakini wachezaji wabunifu kama vile Manuel Lanzini na Sofiane Feghouli wanaweza kuisumbua beki ya Chelsea, Andre Ayew atakuwa anakumbuka kufunga goli lake la  kwanza kabisa kwenye Premier League dhidi ya Chelsea msimu uliopita.

Toa Utabiri wako kuhusu mechi Hii hapa chini mwana Mediahuru!!

Soma na hizi

2 thoughts on “Premier League !! West Ham vs Chelsea Siku ya Jumatatu (Toa Utabiri wako !!!)”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close