Nyingine

Premier League!! Stoke City V Chelsea Siku Ya Jumamosi (Nani Atashinda?? Toa Utabiri Wako)

Stoke City wanaingia uwanjani kupambana na timu inayoongoza Ligi Kuu ya Uingereza kwa sasa Chelsea walifanikiwa kupata clean sheet ugenini walipocheza na  Manchester City, Mark Hughes atakuwa na uhakika na kikosi chake kuelekea kwenye mechi hii pale Bet365 Stadium.

Chelsea wanaongoza ligi kwa point 10 baada ya kupoteza mchezo mmoja tu katikati ya mwezi wa tisa, na Antonio Conte atatumia nafasi hii kujaribu kuwa timu pekee iliyoondoka bet365 Stadium ikiwa na point tatu kwenye ligi tangu tarehe 19 Novemba.

Baada ya Stoke kuanza vibaya msimu huu wa ligi, Hughes ameonyesha maajabu kwa kuipeleka timu juu ya nusu ya msimamo wa ligi , ila sasa anahitaji timu yake iendeleze mapambao na kufikia nafasi ya nane mwishoni mwa mwezi huu wa tano.

Conte ametumia  mashindano ya FA kubadilisha wachezaji wake , ila kikosi chake cha kwanza kinaingia kwenye mechi hii wakiwa tayari wamecheza dakika 90 mwanzoni mwa wiki.

Kwenye robo fainali ya FA Cup , Blues walifanikiwa kuifunga Manchester United ambayo ilicheza na watu 10 karibu nusu nzima ya mchezo, na nimatokeo ambayo yanaendeleza rekodi ya kutokufungwa tangu wikiend ya kwanza ya mwaka 2017.

Habari za Timu-

Conte anaweza kumwanzisha Pedro, ambaye hakucheza kwenye mechi dhidi ya United richa ya kufunga magori matatu kwenye mechi nne zilizopita.

Swala lingine ambalo bado lina waacha watu njiapanda ni kuhusu nani ataanza kati ya Nemanja Matic na Cesc Fabregas kwenye nafasi ya kiungo wa kati.

Hughes amesema atafanya mabadiliko kwenye kikosi cha kwanza ,  richa ya matokeo yao ya hivi karibuni , akijaribu kuendana na mfumo wa  Chelsea 3-4-3.

Kocha huyo amesema Xherdan Shaqiri yupo fit kwa sasa baada ya kuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili , ila Glen Johnson hatakuwepo kukutana na moja ya timu yake ya zamani.

Kikosi kitakachoanza kwa Stoke City: Grant; Bardsley, Shawcross, M.Indi, Pieters; Diouf, Cameron, Allen, Sobhi; Walters, Berahino

Kikosi kitakachoanza kwa Chelsea: Courtois; Azpilicueta, Luiz, Cahill; Pedro, Fabregas, Kante, Alonso; Willian, Costa, Hazard

Ujumbe wa Mhariri-  Mechi hii itakuwa ngumu kwa pande zote mbili. Chelsea wapo kwenye fomu nzuri na nawatabiria ushindi , ila Stoke City wana fomu nzuri wanapocheza uwanja wa nyumbani. Kwa upande wangu mechi itamalizika kwa matokeo ya  Stoke 1-2 Chelsea. Vipi kwa upande wako? 

Toa Utabiri Wako Hapa Chini!!!

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close