Premier League!! Chelsea V Manchester City Siku ya Jumatano (Toa Utabiri Wako!!)


Chelsea inayoongoza Ligi kuu ya Uingereza (Premier League) kesho jumatano wataikaribisha  Manchester City kwenye uwanja wao wa Stamford Bridge mechi ambayo inaweza kufungua tena mbio za ubingwa kwa timu zingine.

The Blues ambao mbio zao za kucheza mechi 12-bila ya kufungwa zilifikia mwisho siku ya jumamosi pale Chelsea ilivyofungwa  2-1 na Crystal Palace wakiwa nyumbani .

Cesc Fabregas alianza kuipatia goli Chelsea ndani ya dakika tano za kwanza, ila baada ya dakika sita timu hiyo ikicheza uwanja wa nyumbani ilikuwa nyuma baada ya kufungwa magoli mawili ya haraka.

Matokeo hayo yamekiacha kikosi cha Conte  kuwa juu ya Spurs kwa point saba, Tottenham watakutana na  Swansea uwanja wa Liberty siku ya Jumatano.

Mechi hii inaweza kuwa nafasi pekee kwa Manchester City kuingia tena kwenye mbio za ubingwa. Ikiwa imebaki michezo 9 tu , kikosi cha Guardiola kipo nyuma kwa point 11 kuwa nafasi ya kwanza.

City walifungana 2-2 na Arsenal siku ya jumapili, Leroy Sane na Sergio Aguero waliifungia timu hiyo.

Mechi ya mzunguko wa kwanza, Chelsea walishinda 3-1. Aguero na Fernandinho   waliondoka na kadi nyekundu huku Diego Costa, Eden Hazard na Willian wakiingia kwenye scoresheet.

Habari za Team –

Victor Moses yupo kwenye tathmini baada ya kuumia mguu . Mchezaji huyo kutoka nchini Nigeria anaweza kurudi uwanjani baada ya kukosa mchezo wa jumamosi.

Kuna uwezekano mkubwa Pablo Zabaleta atarudi kwenye nafasi yake baada ya Jesus Navas kucheza pale Emirates. Bacary Sagna bado yupo kwenye matatizo ya groin.

Ni upi utabiri wako ?? Toa maoni hapa chini!!

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA