Polisi wauawa katika shambulio la kutisha Pwani


Polisi saba waliokuwa doria katika Kijiji cha Jaribu mpakani mwa wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani, wanadaiwa kuuawa usiku wa kuamkia leo kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika.

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo, lakini akasema taarifa zaidi zitatolewa na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Pwani.

Taarifa za uhakika zimeeleza kuwa polisi hao walikuwa kwenye gari wakirejea kituoni kutoka doria na walishambuliwa na watu waliotokea msituni.

Bunduki walizokuwa nazo aina ya SMG zimeporwa. Taarifa zingine zimedai kuwa mauaji hayo yamefanywa na mtu mmoja aliyekuwa na silaha nzito.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA