Nyingine

Polisi wamkamata Tundu Lissu nyumbani kwake Dodoma apelekwa Dar

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu amekamatwa na Polisi nyumbani kwake Dodoma leo Alhamisi 16/3/2017 na kupelekwa katika ofisi ya kamanda wa polisi wa mkoa huo.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa polisi wa mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amesema ni kweli amekatawa na anasafirishwa kwenda Dar es Salaam kwa madai kuwa “ameruka dhamana”.

Lissu ambaye pia ni wakili maarufu nchini, anagombea nafasi ya urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Chanzo: Mwananchi

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *