Nyingine

Pluijm wa Yanga amesaini miaka miwili kuifundisha Singida United

Baada ya picha kusambaa zikimuinesha kocha wa zamani wa Yanga Hans van der Pluijm akiwa na mchezaji mpya (Kutinyu) aliyesajiliwa na Singida United, hatimaye leo March 17, 2017 kocha huyo amesaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo ya mkoa wa Singida iliyopanda kucheza ligi kuu msimu ujao.
Pluijm alikuwa kocha mkuu wa Yanga kabla hajabadilishiwa majukumu na kuwa mkurugenzi wa ufundi baada ya ujio wa George Lwandamina kama kocha mkuu kwenye kikosi cha wanajangwani.

Hali mbaya ya kiuchumi ndani ya Yanga ilipelekea Pluijm kuvunjiwa mkataba baada ya uongozi wa Yanga kupitia kwa katibu mkuu wake Boniface Mkwasa kusema klabu haina uwezo tena wa kuendelea kumlipa.

Tangu March 15 mwaka huu kulikuwa na picha ya Pluijm ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha akimkabidhi jezi Kutinyu aliyekuwa kiungo wa Chicken Inn ya Zimbabwe. Moja kwa moja picha hiyo ikawa ikihusisgwa na Pluijm kujiunga na Singida United.

Jana Pluijm alikanusha habari za yeye kujiunga na Singida United akisisitiza bado alikuwa na offer tatu mkononi na hakuwa amefanya maamuzi atakwenda wapi kwa sababu aliua hajasaini mkataba mahali popote. Mwisho wa siku leo amesaini mkataba wa kuitumukia timu hiyo iliyokosekana VPL kwa muda mrefu.

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close