Q & A: Je PIN ya tarakimu 6 kweli ni salama zaidi kuliko PIN ya tarakimu nne?


Jana katika pitapita zangu mtaani nilikutana na wadau ambao walikuwa wanabishana kuhusu swali hili:

Je PIN ya tarakimu 6 ni salama zaidi kuliko PIN ya tarakimu 4 ?

Mmoja alikuwa anasema tutumie PIN zenye tarakimu nne tu kwa sababu zinatosha kuleta utofauti wa namba za siri baina ya mtu na mtu.

Mwingine akawa anasema ni vyema kutumia PIN yenye tarakimu kwanzia sita kwa sababu inaongeza usalama wa simu na nivigumu mtu mwingine kuijua.

Wote walitaka kujua mimi nakubaliana na nani………

Jibu langu lilikuwa jepesi kama hivi:

PIN ya tarakimu sita sio tu kwamba ni salama zaidi kuliko PIN ya tarakimu nne bali kihalisia ni BORA na salama zaidi. Na hayo sio maoni yangu, ni ukweli wa takwimu. Hii ndiyo sababu …

PIN ya tarakimu 4 ina mchanganyiko 10,000 unaoweza kukisiwa. Najua hiyo inaonyesha kama usalama ni mkubwa, lakini kwa kweli ni rahisi kuijua kwa kutumia mbinu mbalimbali.

Hata hivyo, PIN ya tarakimu 6 ina mchanganyiko unaowezekana wa milioni 1. Hii inafanya kuwa VIGUMU zaidi kuijua (na inatumia muda mwingi zaidi) kwa kutumia mbinu sawa.

USHAURI: Ikiwa unataka kutumia PIN kuweka salama kifaa, debit card au kitu kingine chochote, tumia PIN ya tarakimu 6 itaifanya kazi vizuri zaidi kuliko kutumia tarakimu nne tu.

Maujanja # 1: Chapisho hili linaeleza jinsi ya kugundua (na kuepuka) barua pepe za udanganyifu.

Maujanja # 2: Unataka kuhakikisha hupitwi na vidokezo vyetu? Bonyeza hapa kujiunga na Facebook Page ya Mediahuru!

Je, una swali la teknolojia kwa Wataalam wa Mediahuru? Bofya hapa na ulitume!

Ikiwa umesoma na kuona chapisho hili lina manufaa, unaweza kutusaidia kusmbaza ? Bonyeza tu moja yasocial media sharing buttons hapa chini.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA