Habari za TeknolojiaNyingine

Picha: Vilio Na Simanzi, Msiba wa Taifa, maelfu walivyoaga miili 32 Arusha

Leo ndio miili ya watu 32 wakiwemo wanafunzi 29 wa Lucky Vicent waliopata ajali ya gari May 6, 2017 imeagwa mkoani Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yuko mjini Arusha muda huu ambapo anaongoza wananchi wa mkoa huo pamoja na mikoa ya jirani katika kuuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili pamoja na dereva Mmoja wa shule ya Lucky Vincent iliyopo mkoani humo.

Wananchi wakiwa amejitokeza kwa wingi katika uwanja wa Sheikh Abeid Karume Arusha kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu 2 na dereva mmoja.

Wanafunzi na walimu hao walipata ajali hiyo wakati wanaenda kwenye shule iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mitihani wa ujirani mwema baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia korongoni kwenye eneo la Rhotia wilayani Karatu.

Miili ikishushwa ndani ya gari

Kutoka katika Uwanja wa Kumbukumbuku ya Sheikh Amri Abeid mediahuru.com imekusogezea picha hizi za  baadhi ya matukio uwanjani hapo.

Majeneza yaliyohifadhi miili ya marehemu wakati wa tukio la kuwaga, Arusha
Mama akisaidiwa na watu wa msalaba mwekundu baada ya kuanguka

 

Watu wa Huduma ya Kwanza wakimpatia huduma mmoja wa wazazi walioondokewa na watoto wao, Arusha

 

Baadhi ya viongozi wakiwa katika msiba huo

 

Waombolezaji wakiwa ndani ya Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, Arusha

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close