PF Sense programu ya kukinga virusi kwenye kompyuta yako


Katika dunia ya leo yenye ongezeko la mashambulizi ya mtandao hatuwezi kuishi bila kinga ya virusi. Kinga ya virusi ni mfumo wa usalama wa mtandao wa maunzi ngumu au program tumizi  iliyotengenezwa kukataza  kuingia sehemu iliyozuiliwa ya mtandao.

Katika hali ya kawaida, huduma ambazo hazitakiwi kufikiwa katika eneo dogo la mtandao zimelindwa kwa kinga  ya virusi. Kuna aina mbali mbali nzuri za kinga ya virusi ya maunzingumu inayotumika sokoni, hata hivyo katika hali ambayo bei ni  tatizo, vibadala nafuu kama pfSense vinaweza kutumika.

pfSense ni program tumizi kamili ya kukinga virusi inayotumika katika kompyuta binafsi kutoa huduma zote muhimu kama za  vitumi vya kibiashara. pfSense ina msingi kwenye program tumizi rafiki ya FreeBSD  ikiwa na seva za mtandao LightPD na PHP. Pia pfSense inaingiliana vizuri kimtandao na hivyo kurahisisha usimamizi wake.

SOMA NA HII:  Fahamu Faida & Hasara za Kutumia Kompyuta ya Windows 8

Licha ya uwezo wake wa kukinga virusi, pfSense ina uwezo mkubwa na rahisi wa kufikia sehemu mbalimbali   na  inaweza pia kutumika kama mahali pa kufikia bila waya, kutumika kwenye VPN na  vile vile kutumika kwenye Seva ya DHCP. pfSense inaweza kufanya kazi vizuri kwenye mtandao tata na kuweza kukinga mtandao wako kwa gharama ndogo.

TZ-CERT inakushauri kufikiria kutumia kinga ya pfSense kama mtandao wako hauna kinga ya virusi na  gharama ni tatizo.

Licha ya pfSense kuna kinga za virusi nyingine za kufikiria. Baadhi ni smoothwall na Untangle NG.

Unaweza kujifunza zaidi kuhusu pfSense  katika tovuti yao https://www.pfsense.org

SOMA NA HII:  Q & A: Je PIN ya tarakimu 6 kweli ni salama zaidi kuliko PIN ya tarakimu nne?

Taarifa na TZ-CERT

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA