Sasa unaweza kutumia PayPal kupitia app ya simu ya Skype kutuma pesa


Mtandao mkubwa wa malipo mtandaoni ambao bado unakua, PayPal imetangaza makubaliano mpya na Skype ambayo yatawawezesha watumiaji katika nchi 22 ulimwenguni kote kutuma fedha kwa watumiaji wengine wa Skype kupitia toleo la jipya la app ya simu ya Skype.

paypal-app-ya-simu-skype-kutuma-pesa

Hii inaongeza uwezo wa PayPal kufikia watu wengi zaidi- app ya Skype imepakuliwa mara zaidi ya bilioni hadi sasa, na ina watumiaji wa kila mwezi milioni 300, kwa mujibu wa kampuni mama ya Skype-Microsoft, kama ilivyo mwaka jana.

Ili kutumia kipengele hicho, utaliwa kuwa kwenye toleo la hivi karibuni la app ya simu ya mkononi ya Skype. Kisha, utachagua “Find” kwenye bar ya juu wakati wa kuzungumza na rafiki au mshirika wa familia, na uchague “Send Money”. Unaandika tu kiasi cha kutuma, kuthibitisha malipo, na kisha bonyeza “send” kutuma ili kukamilisha shughuli.

Huduma imetengenezwa kwajili ya kutuma pesa kati ya marafiki na familia – si malipo ya bidhaa au huduma kutoka kwa biashara. Na kama malipo ya PayPal ya peer-to-peer kwenye majukwaa mengine, viwango vinafanana. Hivyo, kutuma ni bure kama unatumia kadi yako ya PayPal au kadi ya debit nchini Marekani. Ikiwa unachagua kutumia kadi ya mkopo (credit card), ada ni asilimia 3.4 ya kiasi unachotuma pamoja na $ 0.30.

Huu ni wa hivi karibuni katika mfululizo wa ushirikiano kati ya PayPal na makampuni mengine ndani ya miezi ya hivi karibuni, zikiwa ni juhudi za kuimarisha msimamo wake dhidi ya vitisho kutoka kwa makampuni kama huduma ya Apple Pay na hata huduma ya U.S. banks , Venmo, Zelle. Na inafanya hivyo kwa kushirikiana na wapinzani wake wa zamani, ikiwa ni pamoja na Apple, pamoja na Visa na MasterCard.

Kampuni hiyo pia hivi karibuni imetangaza ushirikiano na Samsung Pay, Android Pay, na Baidu; Na kupanua makubaliano yake ya kushirikiana na Citi na Chase. Na kwenye upande wa teknolojia ya vitu vingine, PayPal imeanzisha “instant bank transfers”, Siri integration, inaruhusu malipo kwenye iMessage, Slack, na Outlook.com.

Tayari uwezo wa kutuma fedha umeshaanza kufanya kazi kwa watumiaji wa Skype kwenye iOS na Android, Marekani. na mahali pengine.

Orodha kamili ya masoko yaliyounganishwa ni pamoja na: Marekani, Uingereza, Austria, Ubeligiji, Kanada, Cyprus, Estonia, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ugiriki, Ireland, Italia, Latvia, Luxembourg, Malta, Uholanzi, Ureno, San Marino, Slovakia, Slovenia and Hispania.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA