PayJoy Kushirikiana na CBA na Vodacom Kuimarisha Huduma za Kifedha


Fintech startup kutoka San Francisco (PayJoy) imethibitisha kuwa kuna mazungumzo ya ushirikiano yanaendelea kati yao, CBA na Vodacom kusaidia kuimarisha huduma za kifedha nchini Tanzania. Ushirikiano utaimarisha usalama wa watumiaji kupitia aina mbadala za mikopo na utoaji wa mkopo unaofaa. Ushirikiano wa kimkakati unahusisha uzoefu wa watoa huduma, huduma za kifedha, na wataalamu wa teknolojia.

Kwa mujibu wa ripoti ya kampuni hiyo, watumiaji wataweza kulipa mkopo kupitia M-Pawa. Mpango huo unatokana na mfumo wa kibenki wa M-PESA ambao huwawezesha wanachama wa Vodacom kukopa na kuhifadhi fedha kupitia simu zao za mkononi. Wateja wanaweza kununua simu janja zao kwenye maduka ya Vodacom zaidi ya 350 nchini Tanzania baada ya kukamilika kwa mchakato wa ukaguzi. Simu janja ya kipekee itakuwa na programu ya Pay Joy Lock inayozuia apps za simu za mkononi kwa kesi zisizo za malipo. Hata hivyo, kipengele cha Pay Joy Lock bado kinaruhusu kuunganishwa kwa mtandao, upatikanaji wa M-PESA na kupiga simu za dharura.

Doug Ricket, Mkurugenzi Mtendaji wa PayJoy na mwanzilishi mwenza, alibainisha kuwa ushirikiano kati ya Vodacom na CBA utasaidia katika utambuzi wa mpango wa kampuni. Aliongeza kuwa malengo ya kampuni hiyo yanahusisha kufanya simu janja na huduma za kifedha kuwa  rahisi kwa watumiaji wengi. Mkataba huo utahamasisha ukuaji wa uchumi katika taaluma zinazohusishwa na uunganisho wa mtandao nchini kote.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi, alieleza kuwa ushirikiano kati ya CBA na Pay Joy una manufaa kwa Kampuni ya Vodacom. Kwa mfano, hatua hiyo inafanana na malengo ya muda mrefu ya Vodacom yenye lengo la kutumia mifumo ya digitali na kuongeza kasi ya kifedha. Makadirio ya wateja wa Vodacom barani Afrika yanafikia watu milioni 71. Aliongezea pia kwamba ushirikiano unawezesha kampuni kuunganisha watu wengi kwa maisha bora leo na kesho.

Mbali na , CBA na Vodacom, Pay Joy pia inakamilisha ushirikiano na Allied Mobile kuleta simu janja zaidi katika bara la Afrika.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA